Madaktari
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimuudumia mgonjwa hospitalini
hapo. Wafanyakazi wa sekta ya afya ni miongoni wa walio ongezewa
mishahara na serikari katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14. Picha na
Maktaba
KWA UFUPI
Vilevile, mishahara ya watumishi wengine wa umma imeongezwa
kwa wastani wa asilimia 8.41. Waraka namba moja kwa watumishi wa umma
uliotolewa na Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George
Yambesi Julai 2 mwaka huu, unaeleza kuwa marekebisho hayo ya mishahara
yatahusu watumishi wa serikali kuu na watumishi wa serikali za mitaa.
Dar. Serikali imetangaza mishahara mipya kwa watumishi wa
umma itakayoanza kutumika mwezi huu, huku kima cha chini kikiongezwa kwa
asilimia 41.18 kutoka Sh 170,000 hadi Sh240,000.
Vilevile, mishahara ya watumishi wengine wa umma imeongezwa
kwa wastani wa asilimia 8.41. Waraka namba moja kwa watumishi wa umma
uliotolewa na Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George
Yambesi Julai 2 mwaka huu, unaeleza kuwa marekebisho hayo ya mishahara
yatahusu watumishi wa serikali kuu na watumishi wa serikali za mitaa.
Wengine watakaonufaika na marekebisho hayo ni watumishi
walioshikizwa kwenye taasisi za umma na watumishi ambao watakuwa kwenye
likizo inayoambatana na kuacha kazi, kustaafu kazi au kumaliza mikataba
baada ya Julai mosi mwaka huu.
Waraka huo umeonyesha kuwa watumishi wa serikali ambao
wanapata mishahara binafsi isiyo ndani ya viwango vya mishahara ya
serikali hawatahusika na marekebisho hayo.
Mei 29 mwaka huu, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka,
aliliambia Bunge, kwamba Serikali imekamilisha majadiliano ya kuongeza
kima cha chini cha mshahara katika sekta 12 binafsi, kitakachoanza
kutumika rasmi Julai mosi.
Waziri Kabaka alitaja sekta hizo kuwa ni ya Ujenzi, Shule
Binafsi, Nishati, Viwanda na Biashara, Hoteli na Huduma za Majumbani,
Ulinzi Binafsi, Madini, Afya, Uvuvi na Huduma za Majini, Usafirishaji,
Mawasiliano na Kilimo. Kwa mujibu wa Kabaka, mishahara imepanda kwa
kiwango cha asilimia kati ya 21 na 65 huku Afya ikiongoza kwa kuongezwa
ikifuatiwa na sekta ya hoteli na huduma za nyumbani yenye asilimia 55.
Mei mosi mwaka huu akiwa mkoani Mbeya, Rais Jakaya Kikwete,
aliahidi unafuu wa maisha kwa wafanyakazi kwa kuangalia uwezekano pia wa
kupunguza kodi kwenye mishahara, Lipa Kadiri Unavyopata (PAYE).
Kuhusu kuongeza mishahara, Rais Kikwete aliahidi wafanyakazi
wote kwamba Serikali itaendelea kuiongeza kulingana na hali ya uchumi wa
nchi. Waraka huo unaonyesha kuwa mishahara mipya kwa watumishi wa
serikali kada ya masharti (operational service), ngazi ya mshahara na
mshahara mpya kwenye mabano ni;
TGOS A
TGOS A 1. (Sh240,000), TGOS A 2. (Sh245,600), TGOS A 3.
(Sh251,200), TGOS A 4. (Sh256,800), TGOS A 5. (Sh262,400), TGOS A 6.
(Sh268,000), TGOS A 7.(Sh272,000), TGOS A 8(Sh279,000), TGOS A
9.(Sh284,800), TGOS A 10(Sh290,400), TGOS A 11(Sh296,000), TGOS A
12(Sh301,600), TGOS A 13(Sh 307,200), TGOS A 14(Sh312,800), TGOS A 15(Sh
318,400), TGOS A 16(Sh324,000), TGOS A 17(Sh329,600) na TGOS A
18(Sh335,200).
TGOS B
TGOS B 1. (Sh347,000), TGOS B 2. (Sh356,500) TGOS B 3 .
(Sh366,000), TGOS B 4 . (Sh375,500), TGOS B 5. (Sh385,000), TGOS B 6.
(Sh394,500), TGOS B 7. (Sh404,000), TGOS B 8. (Sh413,500), TGOS B 9.
(Sh423,000), TGOS B 10. (Sh432,500), TGOS B 11 . (Sh442,000) na TGOS B
12. (Sh451,500).
Source : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mishahara-mipya-serikalini-2013/-/1597296/1928096/-/item/12/-/wrvv60z/-/index.html
Source : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mishahara-mipya-serikalini-2013/-/1597296/1928096/-/item/12/-/wrvv60z/-/index.html
No comments:
Post a Comment