Habari za uhakika ni kuwa muigizaji maarufu Swahiliwood Salma Jabu(
Nisha) atafutarisha mashabiki wake wakubwa wa kazi zake za filamu kesho
jumapili. Chanzo cha kuaminika kilicho karibu na actress huyo kimesema
kuwa mashabiki hao watakaofutarishwa na Nisha nyumbani kwake kijitonyama
Dar es salaam watatoka katika group yake ya mtandao wa WhatsApp na
tayari kila kitu kipo tayari kwa ajili ya tukio hilo muhimu katika mwezi
huu mtukufu wa Ramadhani. Licha ya kuwa actress maarufu Nisha pia ni
producer wa filamu kupitia kampuni yake ya Nisha's Film Productions na
wiki iliyopita filamu yake mpya ya Tikisa iliingia sokoni. Picha za
tukio hilo utazipata hapahapa Swahiliworldplanet.
Mungu akuzidishie Nisha
BONGO NEWS 4 NEWS#
No comments:
Post a Comment