Pages

Monday

WASTARA ALIPIZA MSOTO WA MUMEWE

WASTARA JUMA.

MSANII mwenye heshima tele kunako gemu la filamu Bongo, Wastara Juma amesema ameamua kulipiza muda aliosota kumuuguza mumewe, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’  kwa kufanya kazi kwa bidii ili aweze kufikia levo waliyopo wasanii wenzake.

Wastara ameiambia Stori 3 kuwa, anafanya kazi yake kwa bidii ambapo anatarajia kutoa muvi tatu kwa mpigo ndipo apumzike kulipiza muda ambao hakufanya kazi hiyo alipokuwa akimuuguza mumewe.
 
“Nimemaliza kushuti filamu yangu ya Shaymaa (Kialama) na sasa naendelea kucheza nyingine walau nilipize muda niliokaa bila kucheza filamu,” alisema Wastara.

BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments:

Post a Comment