
MANCHESTER United na Chelsea zimetoshana nguvu kwa sare ya bila kufunguna kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford.
Mourinho
akiiongoza Chelsea ndani ya Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu
arejee kuikochi timu hiyo, alionekana kama mtu aliyelenga kujihami zaidi
kuliko kusaka ushindi.
Kocha
huyo ‘cha maneno’ akapanga kikosi kisicho mshambuliaji hata mmoja akiwa
ni kocha wa kwanza kufanya hivyo katika histotia ya Ligi Kuu.
Mfungaji
bora wa msimu uliopita Robin van Persie akashuhudiwa akipoteza nafasi
muhimu zikiwa zimesalia dakika tatu kabla ya mchezo kukamilika baada ya
shuti lake kuwababatiza Gary Cahill na John Obi Mikel.
Jose Mourinho hakufanya siri juu ya kuonyesha utashi wake wa kutaka kumsaini Wayne Rooney katika siku saba zijazo.
Akicheza
nyuma ya washambuliaji, kinyume na Mourinho anavyotarajia kumtumia
katika Chelsea, mshambuliaji huyo wa Uingereza, aling’ara vilivyo katika
mechi hiyo ya kwanza kwake kuanza tangu mwezi April.
Rooney
aliyekuwa akihaha uwanja mzima huku akishangiliwa na mashabiki wa pande
zote mbili, alimjaribu kipa Petr Cech katika dakika za lala salama.

Chelsea
tayari imeshuhudia ofa zake mbili za kutaka saini ya Rooney zikipigwa
chini na sasa wanatarajiwa kupeleka ofa ya tatu baadae wiki hii.
Kama
kuna mchezaji aliyeoneka anangeweza kufungua mlango wa magoli basi ni
Rooney lakini hilo halikuweza kutokea na timu hizo zikalazimika kugawana
pointi ambayo kwa namna yoyote ile hakuna upande ambao utasononeshwa na
matokeo hayo.
Kwa
mshangao wa wengi Mourinho akampiga benchi Juan Mata ambaye mashabiki
wa United wangeridhika kumuona akibadilishwa na Rooney. Torres naye
akaanzia benchi.
Kwa
kiasi kikubwa United walitawala mchezo, wakipiga pasi nyingi na
kulisogelea lango la Chelsea kila mara lakini mipango yao ikawa
inatibuliwa na safu ya ulinzi ya Chelsea iliyokuwa ikiongozwa na John
Terrey huku mipira michache ikiishia kwenye mikono Petr Cech.
Moja
ya mashuti mazuri yaliyopigwa kwenye mchezo huo ni lile la Eden Hazard
aliloliachia ubali wa mita 30 lakini likaokolewa na De Gea.
Pande
zote mbili zililalamikia kunyimwa penalti, Cleverley alipiga mpira
ulimogonga mkononi Frank Lampard, huku Ashley Cole akipelekwa chini na
Phil Jones ndani ya box.
Kuingia kwa Torres kulishindwa kuleta mabadiliko yoyote yale.
Kuingia kwa Torres kulishindwa kuleta mabadiliko yoyote yale.
Man
United: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia (Young 67),
Cleverley, Carrick, Welbeck (Giggs 78), Rooney, Van Persie.
Akiba: Anderson, Smalling, Lindegaard, Kagawa, Buttner,Young.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne (Torres 60), Oscar, Hazard (Azpilicueta 93), Schurrle.
Akiba: Essien, Mikel, Lukaku, Schwarzer, Mata.
Akiba: Anderson, Smalling, Lindegaard, Kagawa, Buttner,Young.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne (Torres 60), Oscar, Hazard (Azpilicueta 93), Schurrle.
Akiba: Essien, Mikel, Lukaku, Schwarzer, Mata.
HABARI NA SAID MDOE - Saluti 5
BONGO NEWS 4 NEWS#
No comments:
Post a Comment