Tamasha kubwa la filamu la Dar Filamu Festival.
TAMASHA kubwa la filamu linatarajia kufanyika jijini Dar es salaam kwa kuonyesha filamu za kitanzania kwa siku tatu, huku kwa siku zote hizo kukiwa na matukio maalum kwa ajili ya kujenga tasnia ya filamu Swahilihood, ni mwendo wa burudani kutoka kwako nyota wa filamu Bongo tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama. .
Akiongee na FC mkurugenzi wa Haak Neel Production Godfrey Mahendeka ‘Goddy’ ambaye ni mmoja wa waandaaji wa tamasha hilo amedai kuwa lengo la tukio hilo ni kutoa nafasi na kukuza tasnia ya filamu nchini, na kuwakutanisha wadau mbalimbali kwa kukutana na watayarishaji wa filamu, waongozaji, waigizaji ni tukio la aina yake .
“Tasnia ya filamu inazidi kukua kila siku hivyo ni lazima kuwe na matamasha, tuzo na matukio ya namna hiyo, sisi kama kampuni ya Production tumeamua kwa kushirikiana na Filamucentral kuleta zawadi ya tamasha la filamu sehemu ambayo wapenzi wa filamu wataangalia filamu bure kabisa katika Boti kubwa na kujiona kama wapo theater ni tukio la kipekee,”anasema Goddy.
. Dar filamu Festival limeandaliwa na kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na mtandao mahiri wa habari za filamu Swahilihood, pamoja na kuonyeshwa filamu pia kutakuwa na semina kwa wadau wa filamu Bongo, hakikisha haukosi katika tamasha la filamu katika viwanja vya Posta Kijitonyama.
BONGO NEWS 4 NEWS#
No comments:
Post a Comment