MKALI wa muziki wa bongo fleva nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond
Platinum’, amefunguka mengi juu ya historia ya maisha yake na changamoto
alizozipitia katika safari yake ya muziki mpaka kufikia hapa, katika
semina ya Fursa, iliyoandaliwa na Clouds Fm katika kila mkoa tamasha la
Fiesta linapopita.
Diamond alikuwa ni mmoja wa wasemaji, watoa maada mbele ya mamia ya
wakazi wa Tabora katika kuhamasisha vijana kuzijua fursa na kuzitumia
ili kujiletea maendeleo katika maisha yao.
Kwa mujibu wa Diamond, mwaka 2008 na 2009 alikuwa akifanya kazi katika
kiwanda cha mabegi kilichoko Mikocheni na kulipwa mashahara wa
shilingi 2,000 kwa masaa 8, huku nauli ikimgharimu shilingi 1,000 mpaka
kufika kwao na hapo chakula ni zaidi ya shilingi 1,000.
“Ukimuona mtu ana mafanikio kiukweli ujue amehangaika sana, mimi
katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kama ningelikuja kupanda ndege
kwa kutumia pesa yangu, namshukuru sana Mungu na haya ni matunda ya kazi
ngumu ambazo huwa nazifanya,” alisema.
Msanii huyo aliwataka wapenzi wa kazi zake kufanya kazi kwa bidii kwa
kipindi kifupi ili kufanikiwa katika maisha yao na kuonekana watu katika
jamii na sio kudharaulika.
No comments:
Post a Comment