Msanii bongomovie Irene Uwoya anakuja kwenye TV yako kwa njia nyingine tofauti na ya kiubunifu zaidi.
Duniani kuna mastaa kadhaa ambao wanafanya reality show zao, lakini
Irene Uwoya kupitia ukurasa wake wa Instagram ametoa news kwamba
anaanzisha show yake binafsi kupitia kituo cha Clouds TV ambayo ni
tofauti kabisa na show za mastaa wengine. Undani kuhusu show hiyo ni
kwamba kila kitu humo ndani kitahusu mambo ya nyumba.

Irene na crew yake watakuwa na kazi ya kutembelea nyumba zenye hali
mbaya na kuzifanyia ukarabati ili kuboresha hali ya mazingira ya kuishi
ya muhusika mwenye nyumba au chumba. So, show yake itakuwa inaonyesha
mwanzo nyumba ikiwa kwenye hali mbaya hadi atakapo ikamilisha na huo
ukarabati. Hii picha inamuonyesha akiwa setting ku-shoot sehemu ya show
hiyo.
BONGO NEWS 4 NEWS#
No comments:
Post a Comment