KUMBE STAA WA PRISON BREAK, MICHAEL SCOLFIELD NI SHOGA? HIVI NDIVYO ALIVYOTOBOA SIRI
MUIGIZAJI aliyejipatia umaarufu katika tamthilia ya 'Prison Break'
Wentworth Miller maarufu kwa jina la 'Michael Scolfield' ameamua
kujitangaza rasmi kuwa yeye ni shoga.
Muigizaji huyo ameamua kuweka wazi kitendo hicho baada ya kupokea barua
ya mwaliko wa kuhudhuria tamasha la filamu la kimataifa lililotarajiwa
kufanyika St. Petersburg nchini Urusi
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kupitia mtandao wa 'People.com'
imeweka wazi kuwa Scolfield amekataa mwaliko huyo wa kuitembelea nchi
hiyo kutokana na sheria zao zinazowabana wanaume wanaojihusisha na
ushoga.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya muigizaji huyo kuipokea barua hiyo
ya mwaliko ndipo alipoamua kuijibu kwa kuweka wazi kuwa kitendo cha nchi
hiyo kuweka sheria ya kuwabana mashoga ndio sababu kubwa inayompelekea
kushindwa kuhudhuria tamasha hilo.
"Nashukuru kwa mwaliko wenu, mimi nina asili kiasi ya Urusi ingenipa
faraja sana kuitembelea nchi hiyo, lakini kutokana na sheria zenu mimi
nikiwa kama shoga lazima niukatae mualiko huo" aliandika Scolfield na
kuongezea kuwa."Ninaumiwa kwa kiasi kikubwa na jinsi mashoga
wanavyotendewa na serikali hiyo".
Scolfield alieleza kuwa kutokana na sheria hiyo na jinsi serikali ya
nchi hiyo inavyowachukulia mashoga hao hawezi kushiriki kwa amani kwenye
tukio hilo lililoandaliwa na nchi inayowanyanyasa watu kama wao ikiwa
pamoja na kuwanyima haki yao ya msingi ya kusihi.
Mwezi June nchi hiyo ilianzisha sheria dhidi ya ushoga iliyosainiwa na
rais wa nchi hiyo Vladimir Putin ambayo imezua mijadala ya wazi jinsi
sheria hiyo inavyokataza wapenzi wa jinsia moja.
Wentworth ni muigizaji aliyejipatia umaarufu kwenye tamthilia ya Prison
Break mnamo mwaka 2005 hadi 2009, ingawa ameweza kushiriki pamoja na
kuandaa filamu nyingine tofauti tofauti ikiwemo 'Stoker'.
No comments:
Post a Comment