
Onyesho hilo linalojulikana ‘Fashion Avenue’,
litafanyika Agosti 31, 2013 likitarajiwa kuwaleta pamoja wadau na
wapenzi wa mitindo ndani na nje ya Tanzania ambapo wanamitindo 25
watapanda jukwaani kuonyesha mavazi mbalimbali.
Remtulah ameliambia Starehe kuwa, onyesho hilo
litakuwa la mwaliko pekee na kwamba zaidi ya wageni 500 watajumuika
kushuhudia tukio hilo muhimu katika ulimwengu wa mitindo nchini.
“Kwa wale watakaokosa mwaliko hatukuwasahau,
tumewapa nafasi ya pekee kujionea onyesho hilo kupitia mtandao wa
www.ar.co.tz , ikiwa ni mara ya kwanza nchini onyesho kama hilo
kuonekana kwenye mtandao wa intaneti,” alisema
Remtulah alifafanua kwamba kuonyesha onyesho hilo
kupitia mtandao, itawasaidia mashabiki wengi ndani na nje ya nchi
kushuhudia kila tukio ndani ya onyesho.
Akizungumzia toleo lake jipya , Remtulah alisema kuwa litakuwa na vionjo tofauti na ilivyozoeleka.
“Nguo nilizobuni safari hii ni tofauti kabisa na
zile zilizozoeleka. Ni nguo zinazovalika, lakini nimeziongezea vionjo
zaidi ili kuleta ladha bora itakayokubalika na watu wengi,”
alisisitiza.
Remtulah alisema kuwa mwaka huu ameamua kwenda mbele zaidi na kubuni mavazi atakayoyatangaza kimataifa
zaidi tofauti na ilivyozoeleka kwamba nguo za wabunifu wengi wa
Kitanzania huishia jukwaani.
“Mwaka huu nimepanga kuboresha zaidi mavazi yangu
na kuwa na hadhi ya kimataifa. Hiyo itanisaidia kupata soko popote
duniani,” anasema Remtula.
Alibainisha kwamba ikiwa hilo litakamilika
ataweza kufanya maonyesho mengi nje ya nchi kwa sababu, mbali ya
kuonyesha itakuwa rahisi kwake kuuza hivyo, kuzidi kutambulika duniani.
Kuhusu vyombo vya habari vitakavyoonyesha onyesho
hilo Remtula alisema kuwa kutakuwepo na vyombo vya ndani pamoja na DSTV
watakaorusha onyesho hilo kimataifa.
“Vunja kabati ndio dress code ya Fashion Avenue,” alisema.
MWANANCHI MAGAZIN. BONGO NEWS 4 NEWS#
No comments:
Post a Comment