HABARI zilizochimbuliwa kwa undani zinadai kuwa tayari vigogo wawili
waishio nchini wamebanwa na Jeshi la Polisi Tanzania wakituhumiwa
kumtuma Masogange kupeleka madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.
Agnes Gerald 'Masogange' akiwa na rafiki yake aitwaye Rumy.
Kwa mujibu wa habari hizo, vigogo hao (majina tunayo) walidakwa wiki
iliyopita kila mmoja kwa wakati wake na kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha
Polisi (Central), jijini Dar ambako walihojiwa kwa saa sita.
“Hawa vigogo walikamatwa wiki iliyopita na kuhojiwa kwa masaa sita,
waliachiwa lakini waliambiwa wakihitajika tena wataitwa,” kilisema
chanzo hicho.
Chanzo kikaongeza kuwa, licha ya kuhojiwa na kuruhusiwa kuondoka,
vigogo hao, mmoja alinyang’anywa ‘paspoti’ yake huku mwingine akaunti
zake za benki zikifungwa kwa muda usiojulikana.
Habari zinasema kuwa, kigogo ambaye akaunti zake zimefungwa amekuwa
akihaha kila kukicha kuhakikisha zinafunguliwa kwa sababu hana njia
nyingine ya kuingiza kipato.
Juzi, Ijumaa liliwasiliana na Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana
na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ili kujua uhakika wa madai hayo
ambapo alisema:
“Sisi (polisi) tumekuwa tukifanya mambo yetu kwa siri kubwa, si
rahisi kusema. Tukisema kunakuwa na ugumu kwa sababu mnaandika kwenye
magazeti, matokeo yake uchunguzi unavurugika.
“Mfano wale wasichana (akina Masogange) waliokamatwa Afrika Kusini
wamekuwa wagumu kuwataja waliowatuma kwa sababu hao waliowatuma ndiyo
wanaowategemea kuwawekea dhamana.”
Agnes Gerald na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka
huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton
Park nchini humo wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal
Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
BONGO NEWS 4 NEWS#
Credit: Global Publishers
No comments:
Post a Comment