Pages

Wednesday

Huyu ndiyo mtu tajiri sana kuwahi kutokea duniani.. unajua alikuwa na utajiri kiasi gani?

John Davison Rockefeller ndiyo mtu tajiri sana katika historia ya dunia hadi leo, unaambiwa utajiri wake ukifananisha na hawa matajiri wa karne hii amewaacha mbali kupita kiasi, ukichukua utajiri wa Bill Gates na Carlos Slim ambao wote kwa pamoja wana utajiri wa  billioni 140  bado hawatafikia hata nusu ya utajiri aliowahi kuwa nao huyu jamaa.

Mwaka 2007 mtandao wa Forbes ulirekebisha utajiri wa John Rockefeller baada ya inflation (mfumuko wa bei) na kukadiria kwamba alikuwa na utajiri wa dolla billion 663.4
John Rockefeller alifariki mwaka 1937 May 23 huko Florida akiwa na miaka 97, utajiri wake umetokana sana na biashara ya mafuta ambayo kwa kipindi hicho ndiyo ilikuwa nishati mpya na inahitajika sana, alianzisha kampuni inaitwa Standard Oil Company ambayo iliweza kufanikiwa kutawala soko la mafuta kwa kiasi kikubwa sana, baada ya biashara kwenda vizuri akiwa na ndugu zake wa karibu… John Rockefeller aliweza kuwa Mmarekani wa kwanza kufikisha utajiri wa dola billioni moja.
Zaidi ya biashara, John Rockerfeller alitumia utajiri wake mwingi kwenye ku-invest ndani ya masuala ya utafiti wa kisayansi kwenye mambo ya dawa za binadamu, elimu na kusaidia watu kwenye foundation yake ambapo kwenye research alizowahi kuwekeza pesa zake na kuweza kupata mafanikio makubwa hasa kwenye kutokomeza janga la homa ya manjano kipindi hicho na minyoo inayoitwa hookworm.
Kumbukumbu ya John Rockefeller kwenye sekta ya elimu bado ipo hadi leo kwasababu ndiye mwazilishi wa vyuo vikuu vitatu huko Marekani ambavyo ni University of Chicago, Rockerfeller University na Central Philippine University.
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments:

Post a Comment