Benki ya Azania imejipanga kuanzisha dirisha la kutoa huduma zinazofuata kanuni na misingi ya Kiislam
“Tupo kwenye maandalizi kuanzisha huduma za benki kwa wateja wetu ambao ni waumini wa dini ya Kiislam, baada ya kuanza kutoa huduma kupitia mawakala miezi michache iliyopita,” alisema Singili na kuongeza:
“Tunaamini huduma hii itasaidia kuleta ahueni kwa wateja wetu Waislam. Dhamira yetu ni kuhakikisha wanapata huduma za kipekee zitakazokidhi matakwa yao kikamilifu.”
Alisema benki yake imekuwa ikiandaa hafla za
kufuturisha wateja wake Dar es Salaam na mikoa mingine, ikiwa ni sehemu
ya benki hiyo kujumuika pamoja na wateja wake hususan wakati wa
Ramadhan.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, aliwaasa Waislam nchini kuungana na kufuata misingi ya dini ya Kiislam.
“Waislam inatakiwa tutumie Ramadhan kwa kuzidisha upendo miongoni mwetu. Upendo huu usijengeke kwa Waislam pekee bali hata kwa wasio Waislam,” alisema.#
No comments:
Post a Comment