
Habari ni kuwa Jumatano iliyopita watu walijaa pomoni katika mahakama ya
mwanzo Kawe jini Dar es salaam kwa lengo la kusikiliza kesi ya Wema
Sepetu na pia kumuona actress huyo ambaye anakabiliwa na kesi ya
Kushambulia, kufanya vurugu, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao
meneja wa hotel Goodluck Kuyumbu. Wema aliyepandishwa kizimbani mbele
ya hakimu Bernice Ikanda alifika mahakamani hapo akiwa na msafara wa
magari matatu yaliyokuwa na wapambe wake kwa mujibu wa GPL. Magari hayo
matatu yaliyokuwa yamejaza wapambe wa star huyo yalikuwa ni aina ya Audi
Q7, Toyota Opa na Toyota Hiace. Kesi hiyo iliahirishwa mpaka August 20
mwaka huu itakaposikilizwa tena. Angalia picha............
No comments:
Post a Comment