Hatimaye mwanadada Elizabeth Michael (Lulu) yupo teyari kuachia
filamu yake ya kwanza toka atoke jela, filamu aliyoipa jina la Foolish
age inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 30 mwezi huu.
Akiandika kwenye ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii leo mchana lulu aliandika.
“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya
kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie ya
mpya ya FOOLISH AGE....hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika
katika ukumbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa
muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo
pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO
MOVIE.....
Filamu hii inasambazwa ka kampuni ya PROINPROMOTERS.
Huu utakuwa ni uzinduzi mkubwa wa filamu nchini baada ya msanii
wa upande wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz kufanya shoo kubwa
ya mziki kwenye ukumbi mkubwa na maarufu wa mlimani city jambo ambalo
sio la kawaida kwa wasanii wa filamu na muziki hapa nchini.
BONGO NEWS 4 NEWS#
No comments:
Post a Comment