Star Mwingine Mkubwa Ajitangaza Kuwa Ni Shoga, Ni Mpiganaji Mieleka Maarufu [WWE]
Hii ni habari nyingine
ya kuwaacha watu midomo wazi, na hii ni kufuatia hatua ya Nyota Mieleka
kutoka WWE, Darren Young kuweka wazi kuwa yeye ni shoga.
Kutokana na tabia na mfumo wa Wanamieleka kuunda
matukio ya kutengeneza ili kujipatia 'kiki', hapo awali hatua hii ya
kujitangaza kwa Darren ilidhaniwa kuwa ni utani, lakini kimsingi
imeonekana kuwa hakuna points zozote ambazo angeweza kujipatia kwa
kujitangaza kuwa ni shoga. Darren amesema kuwa
anajivunia hali yake hii na yeye ni mtu mwenye furaha licha ya ma-shoga
kuwa bado ni watu ambao jamii inawachukulia tofauti.BONGO NEWS 4 NEWS#
No comments:
Post a Comment