Pages

Sunday

KILI MUSIC TOUR 2013 YAVUNJA REKODI YA MAHUDHURIO KATIKA UWANJA WA LAKE TANGANYIKA MKOANI KIGOMA! CHEKI PICHA 30 HIZI HAPA


Ziara ya wanamuziki waliofanya vizuri mwaka 2012 maarufu kama Kilimanjaro Music Tour 2013 iliyopewa kaulimbiu ya Kikwetu kwetu imefanyika mkoani Kigoma na kuvunja rekodi ya mahudhurio katika uwanja wa Lake Tanganyika baada ya maelfu ya
wakazi wa mji wa Kigoma na maeneo ya jirani kufurika kwa wingi kuwashuhudia wasanii wakali 12 waliopanda jukwaani. Kivutio kikubwa katika tamasha hilo ilikuwa ni wanamuziki wanne wanaounda kundi la Kigoma All Stars, Diamond, Mwasiti, Linex na Recho kupanda mwishoni na kuimba wimbo wao maarufu wa Leka Dutigite na kupata shangwe kubwa toka kwa mashabiki. Hizi ni baadhi ya picha za matukio yaliyotokea.


 Diamond Platnumz akifanya kufuru jukwaani... Hapo ametengeneza umbo la ndege...


 Profesa Jay wa mitulinga..
 Yahaya unaishi wapi?... yahayaeeeeee..... Lady Jay Dee akikamua.
 DJ Akishusha mkong'oto!
 Linex akiwanyanyua mashabiki kwa mistari yake yenye hisia kali...
 Roma mkatoliki kushoto, Mkurugenzi wa Kili music tour katikati na Mwasiti kulia wakionyesha batasam! A! tabasam la nguvu...
 Fid Q Akiporomosha mistari ya kufa mtu..
 Warembo pia walikwepo...
 DJ Wa kilimanjaro music tour akiwarusha watu wa kigoma.
 Mashabiki wakionyesha ishara ya kumpokea Izzo vizuri...
 Izzo Akifanya yake
 Ben Paul Jukwani
 Izzo busnnes akiwa backsage na kinywaji vuguvugu..
 Mwasiti huyo
 Mwasiti akifanya makeke jukwaani..
 Barnaba boy akikamua..
 Recho akifanya yake

No comments:

Post a Comment