Yawezekana Taifa Stars ikawa haifanyi vizuri kwenye michuano ya
kimataifa kiasi cha kuwa chini kwenye chati za soka barani Afrika na
duniani kwa ujumla lakini jina la Taifa hili limekuwa likitajwa na lina
uhakika wa kutajwa katika level za juu za soka barani afrika, hii ni
kutokana na makubwa yanayofanywa na kijana mwenye umri wa miaka 21 raia
wa Tanzania ambaye ni Mbwana Samatta .
Mchezaji huyu ambaye anacheza nafasi ya ushambuliaji amekuwa akifanya
vizuri sana kwenye klabu yake ya Tp Mazembe ya Nchini Congo DRC kwenye
michuano ya kimataifa na amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye michuano
ya kombe la shirikisho barani Afrika .
Samatta alifunga bao moja kwenye mechi iliyochezwa jana kati ya timu
yake ya Tp Mazembe na FUS Rabat ambapo Mazembe ilishinda 3-0 na mpaka
sasa Samatta amekuwa akifunga kwenye mechi zote nne za michuano hiyo
ambazo Mazembe imecheza hali inayomfanya awe na nafasi kubwa ya kuwa
mfungaji bora wa michuano hiyo wakati ikimalizika baadaye mwaka huu.
Mbwana Samatta akiwa anasaini Autograph za mashabiki wa soka Ivory Coast
ambao walivutiwa na uwezo wake wakati wa mazoezi ya Taifa Stars nchini
humo.
Samatta ambaye Mazembe ilimsajili toka Simba Sports Club ya Tanzania
ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na amekuwa na rekodi
nzuri sana ya kufunga karibu kila mechi ambayo anacheza kwenye klabu
hiyo .
Samatta amefanya watanzania wengi kuwa na shauku ya kufahamu matokeo ya
timu ya Tp Mazembe ambapo mara zote watu huuliza timu hiyo imeshinda au
la na baada ya kuuliza hivyo huuliza tena Samatta amefunga mangapi kwa
kuwa wana uhakika juu ya uwezo wake na rekodi yake ya kuzifumania nyavu.
Ubora wake umemfanya kuishi maisha ya kistaa akiwa nchini Kongo ambapo
mashabiki wa Mazembe wanampenda kiasi cha kutaka kupiga naye picha kila
wamwonapo mtaani na wakati mwingine kutakakusukuma gari lake
wanapoliona.
No comments :
Post a Comment