
Papa Francis
apa Francis, amewatakia Waislamu wote duniani,
sikukuu njema ya Eid el- Fitr huku akiwahimiza kuheshimiana zaidi
kupitia elimu.
“Mwaka huu wa kwanza kama kiongozi wa Kanisa
Katoliki, nimeamua kutuma ujumbe huu kwenu marafiki zangu Waislamu
nikiwa na heshima kubwa. Ninatambua uhusiano, udugu na urafiki baina
yetu sisi,” alisema Papa Francis katika salamu zake.
Makao ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani,
yameulezea waraka huo kuwa ni wa salamu maalumu za Sikukuu ya Eid
al-Fitr inayofanyika duniani leo, baada ya kumalizika kwa Mfungo wa
Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.