Ziara ya wanamuziki waliofanya vizuri mwaka 2012 maarufu kama
Kilimanjaro Music Tour 2013 iliyopewa kaulimbiu ya Kikwetu kwetu
imefanyika mkoani Kigoma na kuvunja rekodi ya mahudhurio katika uwanja
wa Lake Tanganyika baada ya maelfu ya
wakazi wa mji wa Kigoma na maeneo
ya jirani kufurika kwa wingi kuwashuhudia wasanii wakali 12 waliopanda
jukwaani. Kivutio kikubwa katika tamasha hilo ilikuwa ni wanamuziki
wanne wanaounda kundi la Kigoma All Stars, Diamond, Mwasiti, Linex na
Recho kupanda mwishoni na kuimba wimbo wao maarufu wa Leka Dutigite na
kupata shangwe kubwa toka kwa mashabiki. Hizi ni baadhi ya picha za
matukio yaliyotokea.
Diamond Platnumz akifanya kufuru jukwaani... Hapo ametengeneza umbo la ndege...
Profesa Jay wa mitulinga..
Yahaya unaishi wapi?... yahayaeeeeee..... Lady Jay Dee akikamua.
DJ Akishusha mkong'oto!
Linex akiwanyanyua mashabiki kwa mistari yake yenye hisia kali...
Roma mkatoliki kushoto, Mkurugenzi wa Kili music tour katikati na Mwasiti kulia wakionyesha batasam! A! tabasam la nguvu...
Fid Q Akiporomosha mistari ya kufa mtu..
Warembo pia walikwepo...
DJ Wa kilimanjaro music tour akiwarusha watu wa kigoma.
Mashabiki wakionyesha ishara ya kumpokea Izzo vizuri...
Izzo Akifanya yake
Ben Paul Jukwani
Izzo busnnes akiwa backsage na kinywaji vuguvugu..
Mwasiti huyo
Mwasiti akifanya makeke jukwaani..
Barnaba boy akikamua..
Recho akifanya yake
No comments :
Post a Comment