Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

Archive

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

FIESTA 2013:AMINI AMBUSU LINAH JUKWAANI LIVE LIVE-SOMA ZAIDI

No comments



Wasanii lukuki wa muziki wa kizazi kipya usiku wa jana wamewapatia burudani wakazi wa Tabora kwenye show ya Fiesta iliyofanyika

No comments :

Post a Comment

Azam : Kiboko ya vigogo

No comments

 
 
KWA misimu miwili mfululizo ni kama Azam FC imekuwa haina bahati. Imekuwa ikiishia kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na kushiriki Kombe la Shirikisho.
Timu hiyo tajiri yenye kila kitu kinachostahili kuitwa timu ya kisasa ya kulipwa, imejipanga kivingine tayari kwa msimu mpya. Msisitizo wa kocha ukiwa ni kuchukua kombe na kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa vile Shirikisho sasa imetosha.
Kocha huyo Mwingereza, Sterwart Hall hakufanya mabadiliko kwenye kikosi chake lengo likiwa ni kuendeleza makali waliyoanza msimu uliokwisha. “Nataka kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita na kuvunja rekodi ya mwaka uliopita, ndiyo malengo yetu,” anasema Stewart ambaye timu yake ndiyo klabu pekee ya Tanzania iliyokwenda Afrika Kusini kwa mechi za kirafiki na ilidumu huko kwa siku kumi.
Katika mechi za huko, safu ya ushambuliaji ndiyo iliyomwangusha kwa kushindwa kufunga mabao mengi jambo ambalo linaonekana kuwa ni tatizo kwenye kikosi hicho. “Mabao ni tatizo, lakini tutacheza na hesabu tu pamoja na mazoezi na kufanikisha malengo yetu na kila mchezaji atafunga,” anafafanua.
Azam, ambayo Jumamosi iliyopita ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii, itaanza ligi bila wachezaji wake wa kimataifa, raia wa Kenya, Humphrey Mieno anayeumwa nyama za paja na Brian Umony raia wa Uganda anayeuguza maumivu ya enka.
Kikosi cha Azam
Azam ipo chini ya Mkurugenzi Aboubakary Bakhresa na makazi yao ni Chamazi, Mbande, jijini Dar es Salaam, ina miaka sita tangu ilipoanzishwa lakini imekuwa tishio kwa wakongwe Simba na Yanga.
Kwa misimu miwili mfululizo mwaka juzi na mwaka jana, iliwapangua wakongwe hao, ikawaweka pembeni na kung’ang’ania nafasi ya pili kwenye ligi na kuliwakilisha Taifa mara mbili Kombe la Shirikisho.
Pia, licha ya ugeni wao huo ndiyo klabu pekee Tanzania inayomiliki uwanja wao binafsi wa kisasa wenye ‘pichi mbili’, moja nyasi bandia na mwingine una nyasi asilia pamoja na hosteli. Mtibwa ndiyo klabu nyingine  yenye uwanja binafsi wenye nyasi asilia. Hali hiyo inaifaidisha Azam ambayo itacheza mechi nyingi zaidi kwenye uwanja wao wa nyumbani ambao pembeni kidogo zipo hosteli zao zinazotumika kwa kambi.
Stewart anasaidiwa na Kalimangonga Ongala pamoja na Mkenya, Ibrahim Shikanda kwenye benchi la ufundi. Kocha Stewart ambaye kwa hulka yake ni mcheshi, amebainisha kuwa mfumo anaopenda kuutumia ni 4-3-3 ingawa mara nyingine ni 4-2-3-1 na 4-1-2-3.
Nahodha wa timu ni John Bocco ‘Adebayor’ na Himid Mao ndiyemsaidizi wake.  Straika, Gaudence Mwaikimba, ndiye mchezaji mrefu kuliko wote na Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ ni mchezaji mfupi kuliko wote katika kikosi hicho.
Azam itatumia jezi za nyumbani rangi nyeupe na ugenini ni bluu na njano.

Azam haijafanya usajili wowote, lakini imewapandisha wachezaji wanne kutoka timu B ya vijana chini ya miaka 20 ambao ni kipa Aishi Manula, Mudhahir Yahya, Hamad Kadili na Dismas.
Wachezaji wa kimataifa ni pacha kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche na Kipre Bolou, Wakenya Mieno na Jockins Atudo pamoja na Brian Umony raia wa Uganda.
Wazawa ni Mwaikimba, Himid, Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aziz, Bocco, Khamis Mcha, Luckson Kakolaki, Mwadini Ally, Said Morad, Marika Ndeule, David Mwantika, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Sure Boy, Samih Haji, Waziri Salum na Seif Karihe.

No comments :

Post a Comment

Vijana weusi wa Marekani waingiwa uoga

No comments




Sabrina Fulton, mama wa Trayvon Martin

Mama wa Trayvon Martin, kijana Mmarekani mweusi aliyeuliwa Florida mwaka jana wakati akielekea nyumbani, anasema kufutwa kwa kesi ya mwanamgambo wa kulinda mitaa aliyemuuwa kumewafanya vijana wengi weusi wa Marekani kuwa waoga.
Akizungumza na BBC, Sabrina Fulton, alitoa wito sheria inayoruhusu kutumia nguvu ya kuweza kuuwa iwapo maisha yako yako hatarini - anataka ibadilishwe katika jimbo la Florida na kwengineko Marekani.
Bi Fulton amepangwa kuhutubia maandamano yanayofanywa mjini Washington kuadhimisha miaka 50 tangu maandamano maarufu yaliyofanywa mjini humo kudai haki za watu weusi na ambayo yaliongozwa na kuhutubiwa na Martin Luther King.
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

SERIKALI YAKAMATA MADINI YENYE THAMANI YA HELA NDEFU LIVE UWANJA WA NDEGE, CHEKI HAPA

No comments



SERIKALI kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini, imekamata madini ya vito yenye thamani ya Sh bilioni 13.17, yaliyokuwa mbioni kutoroshwa nje ya nchi. Madini hayo yalikamatwa katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini, ikiwa ni pamoja na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro na Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TMAA, Bruno Mteta, alisema madini hayo yalikamatwa kwa kipindi cha kuanzia Septemba 2012 hadi Julai, 2013.

Mteta alisema matukio ya utoroshwaji wa madini yamekuwa yakihusisha wageni zaidi, huku akitaja madini yanayoongoza kutoroshwa kwenda nje ni Tanzanite (vito), Amber, Green Gunnet, Soil and gold, Red gold moon stone na Green Tomalin.

Mteta alisema biashara ya kusafirisha madini nje ya nchi kwa njia za magendo, hivi sasa imeshamiri nchini na kuifananisha na biashara haramu ya usafirishaji wa dawa za kulevya.

“Biashara hii hufanywa sana na raia wa nje, hatukatai watu wasifanye biashara ya madini, lakini wafuate utaratibu unaokubalika.

Zipo kesi zinaendelea mahakamani na kesi nyingine zipo mikononi mwa polisi kwa uchunguzi, lakini zipo kesi tatu tayari hukumu imetolewa na madini kutaifishwa,” alisema Mteta.

Mteta alisema Agosti 20, mwaka huu, raia mmoja wa kigeni (hakumtaja jina wala uraia), alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akiwa na aina mbali mbali za madini yenye thamani ya Sh. milioni 25.32.

Mteta alisema siku hiyo hiyo, TMAA kwa kushirikiana na polisi walimkamata raia mwingine wa kigeni katika makazi yake, Jangwani Beach, akiwa na madini ya vito vya thamani.

Uthaminishaji wa madini hayo unaendelea, japokuwa yanaonekana kuwa na thamani kubwa sana, mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi,” alisema.

Alisema TMAA ipo katika hatua za mwisho kuweka mtambo wa kisasa katika viwanja vyote vya ndege, utakaosaidia kubaini watu wanaotorosha madini kwenda nje ya nchi.

“Ni vigumu sana kubaini mtu akiwa amebeba madini, sababu hakuna sauti inayotoka pale mtuhumiwa anapopita kwenye mashine za usalama kwenye viwanja vya ndege, ikilinganishwa na dawa za kulevya au kitu cha hatari,” alisema.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

DUH, UMEONA PICHA ZA VIDEO MPYA YA DIAMOND ALIYOTENGENEZA AFRIKA KUSINI? NI NOMA ZICHEKI HAPA

No comments



Diamond anatarajia kutengeneza tena vichwa vya habari pale atakapoachia video ya wimbo mpya ‘Number 1′ aliyoshoot mwezi huu nchini Afrika Kusini. Video hiyo ambayo Diamond anasemekana kutumia zaidi ya shilingi milioni 50 kuikamilisha, imetengenezwa na kampuni ya Ogopa Videos ya nchini Kenya. Hizi ni screenshots exclusive walizopata bongo5
Screenshot (08h 17m 55s)
Screenshot (08h 17m 59s)
Screenshot (08h 18m 03s)
Screenshot (08h 18m 08s)
Screenshot (08h 18m 10s)
Screenshot (08h 18m 11s)
Screenshot (08h 18m 13s)
Screenshot (08h 18m 18s)
Screenshot (08h 18m 20s)
Screenshot (08h 18m 23s)
Screenshot (08h 18m 28s)
Screenshot (16h 39m 09s)
Screenshot (16h 39m 11s)
Screenshot (16h 39m 12s)
Screenshot (16h 39m 14s)
Screenshot (16h 39m 16s)
Screenshot (16h 39m 19s)
Screenshot (16h 39m 21s)
Screenshot (16h 40m 39s)
Screenshot (16h 40m 45s)
Screenshot (16h 40m 48s)
Screenshot (16h 40m 49s)
Screenshot (16h 41m 03s)
Screenshot (16h 41m 12s)
Screenshot (16h 41m 23s)

Screenshot (16h 41m 25s)CHANZO : BONGO5
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 MKOANI SINGIDA‏ PICHA ZIPO HAPA.

No comments



 Msanii machachari wa muziki wa bongofleva/filamu Shilole akiimba huku akiwa amebebwa na shabiki wake,huku shangwe na miluzi za mashabiki zikiwa zimetawala kila kona.
 Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kucheza jukwaani,wakionesha umahiri wao wa kukata nyonga mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora na vitongoji vyake,waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi.
 Anajiita Raisi wa Manzese,kutoka  kundi la Tip Top Connections,atambulikae kwa jina la Madee akiwaimbisha mashabiki wake wimbo wake wa NANI KAIBA POMBE YANGU.
Mashabiki wakiitikia kwa pamoja huku mikono yao wakipunga hewani.
Mmoja wakali wa hip hop,Stamina akikamua jukwaani vilivyo mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora na vitongoji vyake waliojitokeza kushuhudia makamuzi ya wasanii mbalimbali wa tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Abdul Kiba,msanii wa muziki wa bongofleva akiimba mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
 Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia mbele ya wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah pichani kati akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu. 
 Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.
 Anaitwa Amin,mmoja wa wasanii mahiri akiwaimbisha mashabiki wake kwenye u kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu. Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
 Wenyewe mashabiki waki wanamuita Baba Levo na yeye kabaki Levo kwenye gemu ya muziki wa bongofleva,ndiye pichani Baba Levo akiwaimbisha mashabiki wake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
 Ni shwangwe tu usiku huu kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Wakali wa kudansi kutoka THT,wakijulikana kwa jina la Makomanda wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
 Wanamuita Mzee wa Masauti,Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wake wa muziki wa dansi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,liinalofanyika  kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 wakiwa wamewasha tochi za simu zao wakiashiria kushoo love ya pamoja
Msanii wa muziki wa bongofleva,Rachael akicheza jukwaani na mmoja wa madensa wake,huku mashabiki wake wakipiga mayowe ya shangwa kuonesha kukunwa vilivyo na msanii huyo.

  2jiachie | 2jiacBONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES