HATIMAYE MCHUNGAJI WA KANISA LA KIPENTEKOSTE ATOA SIRI ALIVYOJIHUSISHA NA UUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA..... SOMA HAPA
Mchungaji Donald Mwakisambwe wa kanisa la Kipendekoste la Kiinjili
Tanzania, kwenye ofisi za gazeti hili wakati akitoa ushuhuda wa kufanya
biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Kinara
wa kimataifa wa kuuza madawa ya kulevya aliyezunguka sehemu mbalimbali
duniani kuuza mihadarati, ameacha biashara hiyo na sasa anahubiri
Injili kupiga vita dawa hizo. Kigogo huyo Mtanzania na mzaliwa wa Mbeya,
ambaye sasa anajiita kiumbe kipya katika Kristo, ni Mchungaji
Macdonald Mwakisambwe wa Kanisa la Kipentekoste la Kiinjili jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na NIPASHE Jumamosi jana,
Mwakisambwe alisema alianza biashara ya unga mwaka 1990 na kuifanya kwa
miaka 10, akisafirisha dawa kwa maelfu ya wateja walioko Afrika, Asia,
Ulaya na Amerika. Alisema katika kutimiza azma hiyo, alitumia pasi za
kusafiria za mataifa mbalimbali zenye majina tofauti, zikimuonyesha kuwa
ni raia wa Msumbiji, Tanzania, Kenya, Namibia, Afrika Kusini na
Namibia.
Alieleza kuwa, kumiliki pasi hizo kulilenga kuficha wanausalama
wasimgundue kuwa ni ‘mzungu wa unga’ aliyekuwa anasafiri nchi mbalimbali
duniani ndiyo maana kila alipomaliza mzunguko aliziharibu pasi hizo .
Alisema mwaka 1999, Yesu Kristo, alimtokea akiwa rumande kwenye gereza
la Industrial Area jijini Nairobi, baada ya kuwasili Kenya akitokea
Karachi, Pakistani akiwa na karibu kilo moja ya kete za heroin tumboni.
Mwakisambwe alisema alipotua Nairobi, alikamatwa na maofisa wa polisi
kadhaa waliomueleza kuwa ni muuza unga wa kimataifa na kuwekwa chini ya
ulinzi kwenye kizuizi cha Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta. “Nilikuwa
na pasi ya Msumbiji yenye jina la Danilo Silva Jalla, licha ya kwamba
ni Mtanzania”,anasema.
Anaongeza kusema kuwa ili kupata pasi hizo, alibadilishwa sura halisi
kwa kujiwekea ndevu za bandia, nyusi na nywele nyingi zilizompa sura
tofauti na muonekano mpya kila alipouhitaji. Alisema pasi hizo zilikuwa
zikitengenezwa na magenge ya wanaojihusisha na madawa hayo ambao wapo
kila mahali na wamewekwa mahsusi kufanikisha usambazaji wa mihadarati
kila sehemu inapohitajika.
Alisema hata hapa Tanzania, kuna magenge hayo ya ‘mafia’ na mtandao huo
unashirikiana na maofisa wa Idara ya Uhamiaji wasio waaminifu.
Mchungaji Mwakisambwe alisema kupitia biashara hiyo, alijenga nyumba
kadhaa zilizoko Dar es Salaam na Mbeya pia alikuwa na utajiri mkubwa wa
magari ya kifahari na mengine ya kutanulia.
Alieleza kwa kirefu jinsi dawa hizo zinavyomezwa na kusafirishwa na
kukanusha madai kuwa yanaingizwa tumboni kupitia njia ya haja kubwa.
Alisema yanamezwa kama vidonge vingine baada ya kufungwa ndani ya vifuko
ya nailoni, kisha kuzungushiwa gundi ya karatasi ya nailoni, kuzongwa
na vipande vya glovu nyepesi ambazo hufungwa kikamilifu na kuchomwa kwa
moto kama pipi kifua ili kuvidhibiti visifunguke na dawa kuyeyuka
tumboni. “Kete zinazomezwa zina ukubwa wa kidole gumba cha mtu mzima na
hutofautiana kwa uzito, zipo zenye gramu 10 na ndogo zina gramu tano.
Ukiwa mzoefu unaweza kumeza hata 100 na kubeba pipi zenye uzito wa kilo moja. ”
Mchungaji huyo ambaye sasa anasema anachohitaji ni kuwaeleza watu kuwa
Mungu hapendi biashara ya madawa na kutangaza wokovu, na kusisitiza kuwa
aliyemuondoa kwenye biashara hiyo ni Yesu Kristo. *Mahojiano kamili
kuhusu jinsi Mwakisambwe alivyoanza kuuza mihadarati, nchi
alizotembelea, majina aliyotumia, familia yake, mtandao wa nje na ndani
alioshirikiana nao na jinsi alivyokutana na Yesu akamuokoa,
zitachapishwa kesho kwenye Safu ya NIPASHE Jumapili ya Anayemulikwa.
SOURCE:
NIPASHE
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**
Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPAKundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
-
Klabu ya Arsenal io mbioni kukamisha usajili wa kiungo wa Real Madrid Mesut Ozil katika siku ya mwisho ya usajili barani ulaya. ...
No comments :
Post a Comment