PAPA FRANCIS ATOA SALAMUZA EID KWA WAISLAMU WOTE DUNIANI
apa Francis, amewatakia Waislamu wote duniani, sikukuu njema ya Eid el- Fitr huku akiwahimiza kuheshimiana zaidi kupitia elimu.
“Mwaka huu wa kwanza kama kiongozi wa Kanisa
Katoliki, nimeamua kutuma ujumbe huu kwenu marafiki zangu Waislamu
nikiwa na heshima kubwa. Ninatambua uhusiano, udugu na urafiki baina
yetu sisi,” alisema Papa Francis katika salamu zake.
Makao ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani,
yameulezea waraka huo kuwa ni wa salamu maalumu za Sikukuu ya Eid
al-Fitr inayofanyika duniani leo, baada ya kumalizika kwa Mfungo wa
Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
“Ujumbe wangu katika mwaka huu ni kuwataka nyote
kuakisi kwa pamoja matendo yetu ya kiimani kama Waislamu na Wakristo na
kukuza ushirikiano na kuheshimiana,” alisema Papa Francis.
Ameongeza: “Kuhusu elimu kwa waumini wetu vijana
wa Kiislamu na Kikristo, hatuna budi kuwalea na kuwakuza wakifikiri na
kuzungumzia namna nzuri ya kuheshimiana katika imani za wenzao na
waumini wao na kuepuka tabia ya kudharau au kubeza imani na mafundisho
ya wengine.”
Kwa kawaida salamu hizo hutolewa na Vatican
kupitia Baraza la Kipapa la Mijadala ya Kiimani, lakini safari hii Papa
Francis ameamua kutuma salamu hizo mwenyewe tangu alipofanya hivyo Papa
Yohane Paul II mwaka 1991.
Papa Francis aliendelea kueleza, “Kuhusu kitu gani tunatakiwa
kuheshimana kama binadamu ni maisha, utu wa mtu na kupatikana kwa
heshima na haki ya mtu.”
Papa Francis alisema watu wa imani mbili tofauti hawana budi kuheshimiana.
Ili kufikia azma hiyo familia, shule, mafundisho ya kidini na aina zote za vyombo vya habari vina wajibu wa kushiriki.
“Tunafahamu kuwa heshima ya mtu ni ya msingi
katika uhusiano wowote wa binadamu, hasa kati ya watu ambao wanakiri
imani za kidini. Kwa maana hii, kwa moyo wa dhati, tutakuza urafiki
wetu.”
Kiongozi huyo wa waumini bilioni 1.2 duniani
alisema kutakiana mema wakati wa sikukuu ni kuheshimiana, ingawa si
kukubaliana kwa kila jambo linalofanyika kwenye imani nyingine.
“Tunashiriki nao katika furaha, hatuzungumzii imani na mioyo yao,” alisema.
BONGO NEWS 4 NEWS#
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**
Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPAKundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
-
Waziri wa uchukuzi Prof. Harrison Mwakyembe amemtaja mshukiwa mmoja wa dawa za kulevya aitaye Nassoro Mangunga, lakini mshuki...
No comments :
Post a Comment