Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

Obama ateua msaidizi wake balozi Tanzania

No comments



Rais wa Marekani, Barack Obama (kushoto) akizungumza na washauri wake waandamizi akiwemo Mark Childress (kulia) ambaye amemteua kuwa balozi mpya wa nchi hiyo hapa nchini. Picha na Ikulu ya Marekani 

  • Obama amefanya uteuzi huo ikiwa ni wiki moja tangu alipohitimisha ziara yake katika nchi tatu za Bara la Afrika, Tanzania ikiwa mojawapo. Pia alizitembelea Senegal na Afrika KusinWashington. Rais wa Marekani Barrack Obama amemteua msaidizi wake wa karibu, Mark Childress kuwa balozi wa nchi hiyo, hapa nchini.

Childress ni msaidizi wa Obama katika Ikulu ya Marekani (White House) akiwa Naibu Mkuu wa Utumishi anayeshughulikia mipango katika Serikali ya nchi hiyo na aliwahi kufanya kazi katika Bunge la Seneti.
Obama amefanya uteuzi huo ikiwa ni wiki moja tangu alipohitimisha ziara yake katika nchi tatu za Bara la Afrika, Tanzania ikiwa mojawapo. Pia alizitembelea Senegal na Afrika Kusini.
Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani jana ilisema nafasi hiyo inahitaji kuidhinishwa na Bunge la Seneti la nchi hiyo. Uteuzi wake unaweza kuwa na maana kubwa katika kutekeleza sera za nje za Marekani.
Katika miaka ya karibuni, Tanzania imeshuhudia ziara za viongozi wakuu wa nchi hiyo nchini ambao ni Bill Clinton, George Bush na Obama.
Kuteuliwa kwa Childress, kunaashiria kwamba Balozi wa sasa wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt anakaribia kumaliza muda wake.
Awali, Childress ambaye aliwahi kuwa msaidizi na msiri wa muda mrefu wa Seneta wa zamani, Tom Daschle, alitarajiwa kushika moja ya nyadhifa mbili katika utawala wa Rais Obama ambazo ni Mkuu wa Utumishi katika Idara ya Huduma ya Afya ya Jamii (HHS) au Naibu Mkurugenzi katika Ofisi ya Maboresho ya Afya katika Ikulu ya Marekani.
Hata hivyo, jina lake liliondolewa katika mapendekezo ya uteuzi wa kuongoza ofisi hizo baada ya kuhusishwa katika masuala ya kodi Februari 2009, hivyo kubaki pasipo na jukumu maalumu.
Pamoja na mkanganyiko uliojitokeza awali kuhusu majukumu yake, Childress alimudu kufanya kazi kubwa katika kuwezesha kupitishwa kisha kutekelezwa kwa mabadiliko makubwa katika sekta ya afya ya nchi hiyo. Aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Utumishi wa Marekani, 2012.
Mwaka 2009, mpigania mabadiliko na maboresho ya sekta ya afya Marekani ambaye sasa ni Seneta, Edward M. Kennedy alimwomba Childress kujiunga na timu yake ya ushauri wa masuala ya afya, elimu, wafanyakazi na pensheni.
Timu hiyo pia ilikuwa na kazi ya kumshauri kuhusu masuala ya mabadiliko ya afya na Childress alikuwa miongoni mwa watu walioshiriki kutoa rasimu ya kwanza ya muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Afya 2009.
Baada ya muswada huo kupitishwa Februari 2010, Childress aliondoka katika kamati hiyo na kujiunga na Idara ya Huduma ya Afya ya Jamii Marekani ambako alikuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo mpya akiwa Kaimu Msimamizi Mkuu wa idara hiyo.

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES