WEMA ATIBUANA NA MENEJA WAKE MARTIN KADINDA
KIMENUKA! Beautiful Onyinye au ‘Madam’ Wema Isaac Sepetu anadaiwa kutibuana na yule meneja wake, mwanamitindo Martin Kadinda kwa kurushiana maneno mtandaoni, Amani limesheheni.
Kwa mujibu wa chanzo makini, ishu ilianzia mbali na kusababisha hali kuwa tete kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na kuibua gumzo la aina yake huku mashabiki wa Wema wakidai yao ni macho tu, kuona nini kitakachojiri.
Chanzo hicho kilitiririka kuwa ‘sosi’ ya kutibuana kwao ni baada ya Kadinda kutundika picha ya nyumba yake akiwa amepaka rangi mpya ambapo baadhi ya watu walimpongeza lakini Wema yeye akaguna bila kusifia kama wengine walivyofanya.
Mpashaji wetu aliendelea kutonya kuwa kitendo cha Madam kuguna kilimuumiza Kadinda na kuanza kumwandikia maneno ambayo yalionekana hayakumpendeza Wema.
“Nilijua tu una kiroho na roho ya hasidi iliyojaa uzandiki,” aliandika Kadinda akimjibu Wema.
Ilidaiwa kuwa maneno hayo yalimpandisha hasira Wema na kuamua kumtahadharisha meneja wake huyo kuwa asimwambie maneno ya aina hiyo katika mtandao wa kijamii unaosomwa na wengi.
“Please don’t talk to me like dat on social network (tafadhali usizungumze na mimi hivyo kwenye mtandao wa kijamii),” aliandika Wema.
Mtoa habari wetu aliendelea kumwaga ‘unga’ kuwa baada ya ujumbe huo kumfikia Kadinda naye alijibu mashambulizi kwa kumwandikia Wema: “Umezoea kuogopwa…anyway cut it short (basi yaishe).”
Ilisemekana kuwa baada ya Kadinda kuandika hivyo, wadau mbalimbali kwenye mtandao huo waliwasihi kuweka tofauti zao pembeni au wazimalize wenyewe na siyo kubishana mtandaoni na kufaidisha wasiohusika.
Baada ya habari hizo kutua kwenye ‘deski’ la gazeti hili, mwanahabari wetu aliwatafuta wahusika kwa njia ya simu ambapo Kadinda alipopatikana na kuulizwa juu ya kutibuana na Madam, alikiri kutofautiana na Wema lakini akadai walishaweka mambo sawa.
“Ni kawaida, hata vikombe vikikaa sehemu moja hugongana lakini namshukuru Mungu kwa sasa tupo sawa,” alisema Kadinda anayemiliki lebo ya mavazi ya Single Button.
Kwa upande wa Wema alipoulizwa juu ya ishu hiyo, alicheka na kusema kuwa wao ni binadamu na si malaika hivyo kukwaruzana ni jambo la kawaida.
“Umenichekesha sana, unajua sisi ni binadamu eeeh… siyo malaika, hayo mambo yaliisha siku ileile na hapa baada ya dakika kumi anakuja (Kadinda) kwa ajili ya kupata chakula cha mchana,” alisema
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**
Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPAKundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
-
Waziri wa uchukuzi Prof. Harrison Mwakyembe amemtaja mshukiwa mmoja wa dawa za kulevya aitaye Nassoro Mangunga, lakini mshuki...
No comments :
Post a Comment