Serikali yapata gawio la Sh bilioni 1
KAMPUNI ya Kuhifadhi Mafuta nchini (TIPER) imekabidhi hundi ya Sh bilioni 1 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya gawio la Serikali katika faida iliyotengenezwa hadi kufikia Desemba 31, mwaka jana. Kampuni hiyo inamilikiwa kwa ubia baina ya Serikali na Kampuni ya Uswisi ya Oryx (OOG), kila moja ikiwa na hisa 50, imekuwa ikilipa gawio kama hilo tangu mwaka 2009 baada ya uwekezaji wa Sh bilioni 8.3 ambao uliwezesha kufanya kazi kwa faida.Kampuni hiyo ililipa gawio la Sh bilioni 1.3 mwaka 2009, bilioni moja katika mwaka 2010 na bilioni 2 katika mwaka 2011.
Akizunguzuma wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi hiyo jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER, Daniel Belair, alisema mchango wa gawio toka katika kampuni hiyo utakuwa chachu ya maendeleo ya uchumi nchini.
“Tunayo furaha kukabidhi hundi hii yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa ni wajibu wetu kisheria kama kampuni. Tunaamini mchango wetu utasaidia kuchochea mchakato wa maendeleo ya uchumi wa taifa kwa ujumla,” alisema Belair.
Alisema TIPER inatarajia kuongeza zaidi uwezo wake wa kuhifadhi mafuta ili kufikia zaidi ya mita za ujazo 290,000 ifikapo mwaka 2015, baada ya uwekezaji wa Dola za Marekani bilioni 12.
Belair alisema hadi sasa TIPER ina kituo kikubwa cha kuhifadhi mafuta nchini chenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo zaidi ya 141,000, ikilenga kufikia mita za ujazo 215,000 kwa siku za baadaye.
“Katika uwekezaji mpya, tenki mbili zenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 36,600 zimeshaongezwa katika robo ya kwanza ya 2013. Kipaumbele chetu kikubwa ni kuhakikisha kuwa bidhaa za mafuta ya petroli zinapatikana katika soko muda wote,” alisema.
Alisema katika mwaka wa fedha wa 2011/2012, kampuni yake ilijikita katika miradi mbalimbali ya kusaidia jamii katika sekta za elimu na afya, ikiwa ni sehemu ya sera ya kampuni yake ya kusaidia jamii inayoizunguka kampuni.
Akipokea hundi hiyo kwa niaba ya Serikali, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, aliitaka kampuni ya TIPER iendelee kufanya kazi kwa juhudi na kuihakikishia bodi ya kampuni hiyo kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada zake.
“Tuna furaha kwa kupata mchango huu wa gawio, kwani ni wakati muafaka. Msisite kuifuata wizara yangu kwa jambo lolote linalohitaji msaada wetu,” alisema
BONGO NEWS 4 NEWS#
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**
Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPAKundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
-
Waziri wa uchukuzi Prof. Harrison Mwakyembe amemtaja mshukiwa mmoja wa dawa za kulevya aitaye Nassoro Mangunga, lakini mshuki...
No comments :
Post a Comment