Mwanasheria Mkuu amgeuka Pinda.
*Awataka polisi wasitumie nguvu kubwa kudhibiti raia
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
MWANASHERIA
Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, amelitaka Jeshi la Polisi
nchini, kuacha kutumia nguvu zilizopita kiasi, pindi linapokuwa
likituliza ghasia.
Amesema, pamoja na kwamba jeshi hilo
linaruhusiwa kisheria kutumia nguvu wakati wa kutuliza ghasia, nguvu
hizo hazitakiwi kuzidi kipimo kwa kuwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Jaji
Werema alitoa kauli hiyo mjini hapa jana, alipokuwa akifungua mkutano
wa mawakili wafawidhi wa Serikali, wakuu wa upelelezi wa makosa ya jinai
wa mikoa na vikosi vingine vya polisi.
“Sheria inaruhusu polisi kutumia nguvu katika baadhi ya maeneo, lakini utaratibu lazima ufuatwe.
“Tusitumie nguvu kubwa kupita kiasi, polisi mmejifunza kutumia
mabomu, bunduki na mmejifunza pia kutumia bunduki na kulenga shabaha,
usimpige mtu kichwani, hilo ni kosa, lenga kwenye mguu,” alisema Jaji
Werema.
Kauli hiyo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, inaonekana
kwenda kinyume na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda dhidi ya wanaokaidi maagizo ya polisi.Katika
maelezo yake wakati akijibu swali na papo kwa papo aliloulizwa wakati wa
Bunge la Bajeti lililopita, Waziri Mkuu Pinda, aliruhusu polisi
wawapige raia pindi wanaposhindwa kutii sheria.
Wakati huo huo,
jana Jaji Werema alilitaka Jeshi la Polisi nchini pamoja na wanasheria
wa Serikali, kuacha tabia ya kuwabambikia kesi raia badala yake watafute
ushahidi wa kutosha.
Alisema kama wanamfahamu mhalifu,
wanatakiwa kutumia akili kwa kumkamata kwa kufuata utaratibu wala siyo
kumbambikia kesi isiyo na ushahidi.
“Katika baadhi ya kesi
tusimkamate mtu kama hatuna ushahidi wa kutosha, tunamkamata mtu siku ya
Ijumaa ili tumkomeshe akae ndani halafu Jumatatu anatoka.
“Unamjua
mtu ni mhalifu, lakini unashindwa kumkamata matokeo yake unambambikizia
kesi ya mauaji, sio vizuri, tuache tabia hiyo,” alisema.
Alisema
kwamba, kama polisi na wanasheria watafanya kazi kwa kufuata utaratibu,
utafika wakati wananchi watajenga imani na vyombo vya dola kwa kuwa
watumishi hao watakuwa wakizingatia maadili ya kazi yao.
Alitaka
pia uwepo ushirikiano wa kutosha kati ya wapelelezi na wanasheria wa
Serikali, kwa kuwa bila kufanya hivyo, hakutakuwa na mafanikio katika
utendaji kazi wao.
“Kipindi hiki ni kigumu, tunahitaji
kushirikiana zaidi kuliko kipindi chochote kingine, wapelelezi na
waendesha mashtaka ushirikiano wenu siyo kitu cha hiari bali ni lazima,
kwani kama hamshirikiani, hatuwezi kushinda vita dhidi ya uhalifu,”
alisema.
Jaji Werema alisema ingawa mawakili wa Serikali wana
mamlaka ya kuondoa kesi mahakamani, hawatakiwi kufanya hivyo bila
kuwasiliana na kamanda wa upelelezi wa mkoa husika, ili kujenga uwazi na
kuondoa mianya ya rushwa.
Aliwataka watendaji hao kuhakikisha
wanakuwa waaminifu katika kutunza majalada ya kesi na kuhakikisha
wapelelezi hao na mawakili wa Serikali wanafanya uamuzi wa haraka.
Alisema
kwamba, kitendo cha watumishi hao kuchelewa kutatua malalamiko ya
wananchi, kinawafanya wananchi wakose imani na vyombo vya dola na hivyo
kuwapo ukiukwaji wa sheria kwa wananchi.
“Jinsi tunavyotenda kazi
zetu, tunaweza kusababisha dola kuchukiwa, halafu ikichukiwa tuwalaumu
waandishi, mimi nawaambia, watuandike tu kama tunakosea.
“Tuwe
makini pia na mawasiliano yetu kwenye magazeti, sisi ni dola,
tusiwasiliane kupitia magazeti, tusitupiane lawama, tuwe na mawasiliano
mazuri kati ya ofisi ya DPP (Ofisi ya Mkurugenzi Mashtaka), Ofisi ya DCI
(Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai) na siyo
kuwasiliana kupitia magazeti,” alisema.
Awali, akizungumza katika
mkutano huo, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Elizer Feleshi,
alisema ofisi yake kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama,
imepokea agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuwataka wahalifu kujisalimisha
na wapo tayari kulitekeleza.
“Tunawaasa wahalifu watumie vizuri
muda wa wiki mbili waliopewa na rais, vinginevyo watajutia vitendo vyao
kwa sababu katika mkutano huu, tutajadili namna ambavyo
tutawashughulikia wale ambao hawatatekeleza amri hiyo ya rais,” alisema.
Alisema
mkutano huo ni miongoni mwa mikutano waliyoanzisha chini ya Jukwaa la
Haki Jinai wenye lengo la kuwakutanisha wadau pamoja kujadili changamoto
katika utoaji wa haki jinai.
Alisema changamoto mojawapo
inayowakabili, ni kupunguza msongamano wa mahabusu na wafungwa
magerezani na kwamba idadi yao imepungua kutoka wafungwa 45,000 mwaka
2003 hadi wafungwa 33,033 kufikia Julai mwaka huu.
Pamoja na hayo, alisema uwezo wa magereza yote nchini ni kuhifadhi wafungwa 29,552.
BONGO NEWS 4 NEWS#
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
-
Kundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
-
-
Waziri wa uchukuzi Prof. Harrison Mwakyembe amemtaja mshukiwa mmoja wa dawa za kulevya aitaye Nassoro Mangunga, lakini mshuki...
No comments :
Post a Comment