Jeshi la Polisi mkoani Iringa likimkamata...Freeman Mbowe, pamoja na wabunge watatu kwa muda wa saa tano Iringa.
WAKATI Jeshi la Polisi mkoani Iringa likimkamata na kumshikilia
kwa muda wa saa tano kisha kumwachia huru Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, pamoja na wabunge
watatu, kiongozi huyo amesema kuwa endepo kesi hiyo itafikishwa
mahakamani itakuwa ya 10 kufunguliwa na jeshi hilo.
Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na vilevile
mbunge wa Hai alikamatwa jana asubuhi pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Kambi
hiyo, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa
Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Diwani wa Kata ya Mitimirefu,
Frank Nyalusi, wakidaiwa kuzidisha muda wa mkutano.
Akizungumza na gazeti hili jana, muda mfupi baada ya kuachiwa alisema
kuwa kesi hizo kamwe haziwezi kukiyumbisha chama hicho na badala yake
zimewazidishia mori ya kufanya mageuzi ya kisiasa nchini ili kuondoa
minyororo ya ukiukwaji wa haki.
Alisema kuwa amekuwa akikamatwa na kufunguliwa kesi za ajabuajabu na
jeshi la polisi katika maeneo mbalimbali nchini wakati akifanya
operesheni za kueneza chama mikoani.
Naye Lissu alizungumzia tukio hilo la kukamatwa kwao akisema
limefanyika kisiasa kwa maagizo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya
kamanda wa polisi kuagizwa na wakuu wa mkoa na wilaya.
Lissu alifafanua kuwa kisheria hakuna kosa la jinai kama hilo kwa wao
kupitisha muda wa mkutano na kwamba endapo kulikuwa na uvunjifu wa
sheria walipaswa kukamatwa siku ileile walipotelemka jukwaani.
“Hapa hakuna kosa ni siasa tu za kuelekezwa na CCM halafu polisi wanafuata maelekezo tu.
“Hata maelezo waliyotuandikisha hawaonyeshi kifungu chochote cha sheria tulichovunja.
“Sheria ya vyama kutozidisha muda iko kwenye masuala ya mikutano ya uchaguzi, huu si mkutano wa uchaguzi,” alisema.
Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao, kamanda wa polisi mkoa wa
Iringa, Ramadhan Mungi, alisema kuwa walizidisha muda wa mkutano wa
hadhara uliofanyika juzi katika viwanja vya Mwembetogwa kwa zaidi ya
dakika 25.
“Kutokana na kitendo hicho tumewashikilia na kuwahoji na wakithibitika
kutenda makosa hayo jeshi la polisi litawafikisha mahakamani kujibu
tuhuma hizo,” alisema.
Alisema kitendo cha kuzidisha muda ni kinyume cha sheria na kwamba
CHADEMA waliomba kibali cha kufanya mikutano mitatu mkoani hapa, ratiba
yao ilielekeza kuwa wangefika wilaya Mufindi na kuanza mkutano saa 4:00
hadi 6:00 lakini wakafika saa 9:20 alasiri.
Mungi aliongeza kuwa hata mkutano wa wilayani Kilolo waliotakiwa
kuhutubia saa 6:00 hadi 8:00 mchana wao walifika saa 4:45 na kuhutubia
hadi saa 11:20.
Alisema kuwa Iringa mjini waliomba kuanza mkutano wao saa 8:00 mchana
lakini wakaanza saa 9:00 alasiri kumaliza saa 12:25 jioni zikiwa ni
dakika 25 zaidi ya muda, kitendo alichokiita ni uvunjwaji wa sheria za
nchi.
Katika mkutano huo uliofanyika juzi katika viwanja vya Mwembetogwa,
Mbowe kabla ya kuanza kuhutubia alilitaka radhi jeshi la polisi kwa
kuchelewa kuanza kwa mkutano huo na mara baada ya kumaliza aliomba tena
radhi.
“Nalishukuru sana jeshi la polisi kwa kuonyesha ustaarabu kwa kuwa
niliwaomba radhi kwa kuchelewa kuanza na naomba dakika 10 nyingine
niweze kumalizia jambo muhimu sana kuhusu mchakato huu wa rasimu ya
Katiba,” alisema Mbowe na kuwataka wananchi waliohudhuria mkutano huo
kuwapigia makofi polisi.
Awali akiwa wilayani Kilolo, Mbowe alisema kuwa suala la serikali tatu
halikwepeki kwani ndilo litaweka utaratibu mzuri wa kunufaika na
rasilimali za taifa kwa pande zote mbili za Zanzibar na Tanganyika.
Aliwataka wananchi kuacha tofauti zao za kisiasa ili kuweza kujadili mambo yaliyo muhumu katika rasimu ya katiba.
Mbowe aliongeza kuwa majadiliano ya rasimu ya katiba mpya hayapaswi kufanyika kwa kificho kwa kuwa ni mali ya Watanzania wote.
“Tunapozungumza suala la Katiba ya nchi yetu tuache dini na tofauti
zetu pembeni ili tuweze kutengeneza Katiba nzuri. Wananchi wanapaswa
kushirikishwa,” alisema.
Alisema katika taifa kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa
wananchi ambao unasababishwa na baadhi ya watu kujigeuza kuwa miungu
watu.
“Tunataka kila mmoja awe na haki ya kumiliki ardhi badala ya watu
wachahe kuhodhi kila kitu. Tumeona kuna watu wachache wanataka
kutengeneza Katiba inayowalinda wao.
Tunapozungumzia utawala
hatumzungumzi Kikwete bali tunataka kuweka utawala ambao kila mtu
atakayeingia madarakani aweze kufuata taratibu hizo,” alisema.
Kwa Katiba tuliyo nayo leo tunaweza kuwa na Rais chizi akaipeleka nchi kichizi hivyo hivyo na itabidi tukubali tu.
Alisema Katiba mpya itaweza kuwabana wabunge watakaochaguliwa ili
waweze kurudi kuwatumikia wananchi wao badala ya kuhamia na kuishi Dar
es Salaam.
“Watawala wetu siku hizi wanafanya mambo ya siri. Wanasaini mikataba
ya siri, wanauza madini na gesi kwa siri na kufanya nchi kama ni mali
yao. Katiba mpya itayamaliza mambo ya siri na kila mmoja atajua
kinachoendelea,” alisema.
BONGO NEWS 4 NEWS#
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**
Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPAKundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
-
Klabu ya Arsenal io mbioni kukamisha usajili wa kiungo wa Real Madrid Mesut Ozil katika siku ya mwisho ya usajili barani ulaya. ...
No comments :
Post a Comment