Mwanajeshi JWTZ auawa Kongo
MKUU WA MAJESHI YA ULINZI JENERALI DAVIS MWAMU NYANGE |
Mashirika. Mpiganaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ
Khatibu Mshindo aliuawa kwa kupigwa bomu juzi na waasi wa M23 kwenye Mji
wa Goma ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya
kuzuka mapigano makali.
Wakati Mshindo ambaye alikuwa miongoni mwa askari wa Tanzania wanaounda Jeshi la Umoja wa Mataifa akifikwa na mauti, wapiganaji wengine 10 walijeruhiwa.
Wakati Mshindo ambaye alikuwa miongoni mwa askari wa Tanzania wanaounda Jeshi la Umoja wa Mataifa akifikwa na mauti, wapiganaji wengine 10 walijeruhiwa.
Askari wa Tanzania na wale wa Afrika Kusini wako DRC kwa kazi ya kulinda amani. Malawi bado haijapeleka majeshi yake.
Meja Mshindo alikuwemo katika kikosi cha vifaru na alikuwa kwenye Kambi ya 83KJ iliyoko Kiluvya Dar es Salaam.
Kuuawa kwa askari huyo kumekuja ikiwa ni siku 47
tangu kuuawa kwa askari saba wa Tanzania waliokuwa wakilinda amani
kwenye Mji wa Darfur Sudan na Kikundi cha Janjaweed.
Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba alikiri kutokea
kifo hicho na kusema: “Jana (juzi) Agosti 28, Wanajeshi wetu wakiwa
katika eneo lao la ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na
kusababisha majeruhi.
“Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa
bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki
dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea
vizuri.”
Habari zaidi kutoka Congo zinaeleza kuwa mwili wa
marehemu Meja Mshindo ulisafirishwa jana kupelekwa Entebbe, Uganda
ambako ungefanyiwa matayarisho ya mwisho na tayari kwa kuletwa nyumbani.
Katika hatua nyingine, Askari wawili wa Umoja wa
Mataifa, mmoja akiwa Mtanzania na mwingine raia wa Afrika Kusini
walijeruhiwa kwa bomu eneo la Munigi huko Congo.
Bomu hilo lilirushwa na waasi wa M23 kuelekezwa
kwa askari wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wakikagua maeneo mbalimbali
karibu na Mji wa Goma.
Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban
Ki-moon amelaani mashambulizi na mauaji hayo ya askari huyo wa Tanzania
na kusema: “Ninatoa pole kwa Watanzania na familia ya mpiganaji huyu na
ninalaani kwa nguvu zote mauaji haya na majeruhi kwa walinzi wa amani.”
Msemaji wa UN, alisema Majeshi ya UN kwa
kushirikiana na yale ya Serikali, yalianzisha mapigano makali dhidi ya
waasi wa M23 kwenye eneo la Kibati Kaskazini mwa Goma, kwenye Mji wa
Kivu ya Kaskazini.
Majeshi ya UN na Fardc yalitumia helikopta, vifaru na askari wa miguu
kutekeleza mashambulizi hayo yaliyojibiwa na waasi. Kwa mujibu wa
msemaji huyo, mapigano bado yanaendelea. BONGO NEWS 4 NEWS#
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**
Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPAKundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
-
Klabu ya Arsenal io mbioni kukamisha usajili wa kiungo wa Real Madrid Mesut Ozil katika siku ya mwisho ya usajili barani ulaya. ...
No comments :
Post a Comment