Chidi Benzi akiri kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu na sasa ameamua kuachana nayo baada ya kupata matibabu nchini Kenya na sasa ameachia pini jipya
Jana kupitia kipindi cha xxl cha clouds fm B12 na fety walikua waki hojiana na Chidi Benz naku kiri kutumia madawa ya kulevya soma hapa kujua zaidi.
Rapper Chidi Benz amekiri kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu, na
baada ya kuzidiwa nayo ameamua kuachana nayo na kupatiwa matibabu
Nairobi, Kenya.
Chidi amekiri leo hii kupitia kipindi cha XXL pale alipofika kwa ajili
ya kuachia wimbo wake mpya ambao amewaachia mashabiki kuupa jina lake.
hidi alianza kufunguka mara baada ya kuulizwa na Fetty kuhusu ngoma hii ambayo imefanyika ndani ya wiki moja wakati alikuwa kimya mda ina maana alikuwa harikodi au?
Chidi Benzi: ngoma nimefanya nyingi sana, zingine nimetoa lakini
zilikuwa hazina nguvu sana kwasababu usimamiaji ulikuwa chini na kipindi
kile kulikuwa kuna mambo mengine ambayo tulikuwa tunahusika nayo
yanakuchanganya akili unakuwa unafikiria mawazo mengi lakini usambazi tu
na wewe mwenyewe kujiweka kikazi nilikuwa siko hivyo.
Fetty: Ulikuwa unawaza nini ambayo ilikuwa inakuchanganya akili?
Chidi Benzi: eeeh mambo mambo tu mavitu mengi unajua binaadam
unakua unakutana na vitu unaonana navyo unaungana na vitu unapishana
navyo, kwahiyo vitu vitu tu.
B12: Ok kama unafikiri kwamba inaweza kutusaidia kushare na sisi au kama ni ersonal tunakuruhusu uiweke iwe personal?.
Chidi Benzi: Aaah naweza kushare kwasababu tu familia iliniambia
nisizungumzie sana ila naweza nikashare kwasababu nilikifanya na
nikaamua watu wote wapate hisia kuwa Chidi amefanya, ofcourse nilikua
najihusisha na vitu vingi ambavyo ni vilevi na nini, nilikuwa nikitumia
vitu vingi sana kwahiyo utumizi ule ulikuwa unanifanya saa zingine
nakuwa na hasira na mawazo mengine tofauti tofauti, namchukia kila mtu
na nini, kwasababu natumia vitu mbavyo vinavyozidi, naweza tukaongea na
wewe b12 hivi story lakini nitoka pale namwambia B12 snich tu yaani
unakuwa na anger unakuwa na hasira, kwahiyo sasa dakika ya mwisho
nikagundua naficha watu au naamua kwenda kufanya kitu kwaajili ya afya
yangu na maisha yangu.
B12: Mimi namaindi kujua ni vilevi vya aina gani ambavyo unavizungumzia hapa?
Chidi Benz: aaah pombe, ganja madawa na vinginevyo vinginevyo
B12: kwahiyo unataka kuniambia pamoja na kwenda Nairobi pia ulikuwa umekwenda rihab pia.
Chidi: No sikua rihab ndo maana huwa sitaki kuizungumzia wala
kupost kwenye ma website na nini, lakini ni kama nilienda then baada ya
kufika nikakutana na Nonini kutoka airport tu gari linaanza kwenda
nikagundua kwanza sikufatilia kama ulikuwa ni muda wa baridi kwahiyo
nikagundua kuna baridi, then jamaa anaanza kuniambia yooo unajua tuna
show kama saba, nane tisa kumi, kumi na mbili, nikamwambia show ngapi?
umeniambia show kama tatu tu, akasema eeh nilikuwa nataka tu uje
tunashow kama 7 nane yaani show nyingi, utaweza au unadhani kuna vitu
ambavyo utavihitaji ambavyo itakuwa ngumu kwako?
nikamwambia yaaah kuna vitu nitavihitaji, mimi bana kuna vitu
navyovitumia nimefikia nikikaa twenty minutes bila hivyo vitu ni noma
yaani ni noma nachanganyikiwa nakuwa akili tena sina, kwahiyo sijui
tutafanyaje.akaniambia Chidi na mimi unanijua, unajua yeye nikama
anakunywa pombe lakini siku mojamoja sasa unajua mi ntapaje Chidi na
nairobi ni gharama,
nikamwambia ok, nikamwambia lakini pia nnawazo lingine kuna mtu
alinitonya kuwa kunakitu ambacho kinaweza kufanyika ni pensa nyingi kama
milioni 15 , 16 hivi za kibongo, kama kikifanyika hicho basi
nanyofolewa kabisa hivyo ambavyo vilikuwa vinanifanya niwe hivyo,
akaniambia hiyo naijua lakini ni process ndio maana dunia nzima
hawafanyi hiyo unaskia watu wanakufa daily na madawa hawafanyagi hiyo
wewe je?
nikamwambia mi nafanya kwasababu sasa nishakutana na vitu vingi kama ni
maumivu, ni ishu aibu nishakuta nazo za mapenzi za maisha kawaida
ntashindwa kufanya hicho, akaniambia watu huwa wanakufa sometimes
ikikuzidia, nikamwambia ntafanya si kuna hospitali ni dawa nitafanya.
hela ikapatikana nakumbuka tuka arrange, daktari kaja kanitibia fresh,
kwahiyo mi sijaenda rihab wala sijatumia methadon sijui maana zile ni
mradi tu.
Fetty: ulitibiwa kwa njia gani?
ni dawa ambayo inanunliwa na unachomwa kama mgonjwa tu, yenyewe
inakusafisha wewe pale ambapo ulikuwa ukivuta inaenda kukaa, then baada
ya dakika kadhaa pakikauka panakua pakavu, ni kama ile sehem inakua ni
mbichi ukivuta, lakini ukiwa huna hela huvuti panakuwa pakavu pakikauka
ndio unachanganyikiwa unaanza sasa kuwa na alosto, lakini kama
ukiendelea kuvuta panakuwa pabichi unaendelea, so yenyewe inaenda ni
kama mapovu, panasafisha panakuwa empty ni wewe mwenyewe uamue uendelea
kuvuta ama uache kabisa, lakini yenyewe inakusafisha pale kote, unaanza
kuwa na power, inakupa akili, uso, rangi ya uso, mwili unaanza
kubadilika, unaanza kuwa fine.,,,,,,,so niko fresh, niko healthy, nakula
naishi vizuri naskia vizuri na nime-calm down.
sikiliza ngoma mpya ya Chidi hapa chini, na ushauri wako wa jina unahitajika sana so tupia comment yako hapo chini.
CREDIT:DJ FETTYBONGO NEWS 4 NEWS#
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**
Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPAKundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
-
Waziri wa uchukuzi Prof. Harrison Mwakyembe amemtaja mshukiwa mmoja wa dawa za kulevya aitaye Nassoro Mangunga, lakini mshuki...
No comments :
Post a Comment