Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

Archive

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

HAYA NDO MAMBO YA KUZINGATIA KWA MWANAMKE, PALE UNAPOAMUA KUVAA SHATI LA KITENGE

No comments
solange kitenge shirt
Kitenge ni miongoni mwa mavazi ya Kiafrika yenye heshima ya kipekee. Tofauti na aina nyingine za vitambaa, kitenge kina sifa ya kuvaliwa na watu tofauti tofauti na kuleta maana kwenye mitindo.
Katika kuonyesha thamani yake, wabunifu wa mitindo wameenda mbele zaidi na kubuni hadi mapambo ya kitenge. Leo hii si jambo la ajabu kuona makembe, mikoba na hata viatu vya kitenge.
Kwa miongo kadhaa sasa imeshuhudiwa kitenge kikivaliwa katika mitindo kadha wa kadha. Kwa mfano magauni, makoti, blauzi na hata sketi
. Kadri siku zinavyozidi kwenda mitindo ya vitenge ya aina mbalimbali imekuwa ikibuniwa. Ubunifu huu umekuwa ukiongeza zaidi thamani ya kitenge na hata kukifanya kukubalika na kutambuliwa nje na ndani ya nchi kama vazi la Kiafrika.
url
Kuvaa kitenge kunatosha kabisa kuonyesha ni kwa jinsi gani unajali na kulinda utamaduni wa mwafrika.
Katika kipindi cha hivi karibu wabunifu hao walikuja na shati la kitenge kwa wanawake. Na kabla ya kuyaingiza sokoni walionyesha kupitia maonyesho kadhaa ya mitindo jinsi ya uvaaji wake.
Leo hii imeweza kueleweka vizuri kuwa vazi la kitenge linaweza kutengenezwa shati litakalovaliwa na mwanamke, katika shughuli zake za kiofisi.
Kama ilivyo kwa aina nyingine ya mashati, mashati aina hii yana utaratibu wake katika uvaaji Je, ungependa kufahamu?
Fahamu rangi yako
Kwanza kabisa unatakiwa kujua rangi yako, kwa kujua rangi yako itakuwa ni rahisi kwako kupata ushauri kuhusiana na rangi inayoendana na wewe.
Elewa umbo lako
Usivae shati kwa kuwa tu umemuona mwenzio amevaa. Kabla ya kuvaa hakikisha unajiuliza maswali mawili matatu kuhusiana na umbo lako. Je, linaendana na aina ya shati ulilochagua. Ikiwa wewe ni mnene chagua shati lenye rangi ya giza lakini ikiwa una umbo jembamba si vibaya ukichagua rangi ya kuwaka.
Oanisha shati lako na vazi la chini
Licha ya ukweli kuwa aina hii ya mashati inaendana na suruali na sketi, Lakini ukweli ni kwamba si watu wote wanapendelea sururali au sketi. Hakikisha unachagua vazi linaloendana na mwili wako.
Chagua viatu sahihi
Ni kweli kabisa kila mtu ana viatu vyake anavyopendelea. Lakini ukiwa katika aina hii ya mashati unashauriwa kuvaa viatu vile vitakavyokuweka huru zaidi.
CREDIT:FRESH 121 MEDI BLOG
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES