Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

Archive

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

Shoo ya Ally Remtulah ‘live’

No comments

 
mavazi Ally Remtulah, anarajia kuzindua toleo lake jipya la AR 2014 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Onyesho hilo linalojulikana ‘Fashion Avenue’, litafanyika Agosti 31, 2013 likitarajiwa kuwaleta pamoja wadau na wapenzi wa mitindo ndani na nje ya Tanzania ambapo wanamitindo 25 watapanda jukwaani kuonyesha mavazi mbalimbali.

 
Remtulah  ameliambia Starehe kuwa,  onyesho hilo litakuwa la mwaliko pekee na kwamba zaidi ya wageni 500 watajumuika kushuhudia tukio hilo muhimu katika ulimwengu wa mitindo nchini.
“Kwa wale watakaokosa mwaliko  hatukuwasahau, tumewapa nafasi ya pekee kujionea onyesho hilo kupitia mtandao wa www.ar.co.tz , ikiwa ni mara ya kwanza nchini onyesho kama hilo kuonekana kwenye mtandao wa intaneti,” alisema
Remtulah alifafanua kwamba kuonyesha onyesho hilo kupitia mtandao, itawasaidia mashabiki wengi ndani na  nje ya nchi kushuhudia kila tukio ndani ya onyesho.
Akizungumzia toleo lake jipya , Remtulah alisema kuwa litakuwa na vionjo tofauti na  ilivyozoeleka.
“Nguo nilizobuni safari hii ni tofauti kabisa na zile zilizozoeleka. Ni nguo zinazovalika, lakini nimeziongezea vionjo zaidi ili kuleta ladha bora itakayokubalika na  watu wengi,” alisisitiza.
Remtulah alisema kuwa mwaka huu ameamua kwenda mbele zaidi na kubuni mavazi atakayoyatangaza kimataifa zaidi tofauti na ilivyozoeleka kwamba nguo za wabunifu wengi wa Kitanzania huishia jukwaani.
“Mwaka huu nimepanga kuboresha zaidi mavazi yangu na kuwa na hadhi ya kimataifa. Hiyo itanisaidia kupata soko popote duniani,” anasema Remtula.
Alibainisha kwamba ikiwa hilo litakamilika  ataweza kufanya maonyesho mengi nje ya nchi kwa sababu, mbali ya kuonyesha itakuwa rahisi kwake kuuza hivyo, kuzidi kutambulika duniani.
Kuhusu vyombo vya habari vitakavyoonyesha onyesho hilo Remtula alisema kuwa  kutakuwepo na vyombo vya ndani pamoja na DSTV watakaorusha onyesho hilo kimataifa.
 “Vunja kabati ndio dress code ya  Fashion Avenue,” alisema.
MWANANCHI MAGAZIN.
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES