Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

Archive

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

Ponda azua taharuki

No comments

TAHARUKI kubwa imezuka jana baada ya taarifa mbalimbali kuzagaa kuwa Katibu wa Taasisi na




Jumuiya ya Kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda, amepigwa risasi wakati akitoka katika mhadhara uliofanyika katika viwanja vilivyo karibu na Msikiti wa Dini Moja Mungu Mmoja mkoani Morogor

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zilizozagaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya watu waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili, zilisema kuwa tukio hilo lilitokea wakati kiongozi huyo alipoambatana na wafuasi wake wakielekea katika swala ya magharibi ndipo alipozungukwa na magari matatu ya polisi na kutaka kuondoka naye.
Taarifa hizo zilidai kuwa kiongozi huyo hakuwa tayari kutekeleza amri ya kuondoka na askari hao ndipo walipolazimika kutumia nguvu na kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya wafuasi hao.
“Tukio limetokea kweli na kulikuwa na matumizi ya nguvu ikiwemo mabomu ya machozi na ufyatuaji wa risasi kutoka kwa askari polisi lakini mhadhara wake haukuwa na fujo yoyote,” walisema watoa taarifa hao.
Kwa mujibu wa taarifa zilizozagaa zilisema kuwa polisi walifyatua risasi zilizompata kiongozi huyo begani lakini wafuasi wake walifanikiwa kumtorosha.
Zilisema kuwa kiongozi huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa kutumia usafiri wa pikipiki huku akiingizwa kwa kutumia geti la nyuma la hospitali hiyo.
Hata hivyo taarifa hizo zilisema kuwa Sheikh Ponda aliondolewa muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo na kukimbizwa kusikojulikana.
Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema kuwa taarifa nyingi zimeenea lakini wao kama Jeshi la Polisi hawana taarifa za kiongozi huyo kupigwa risasi.
Shilogile alisema kuwa polisi walikwenda kumfuata wakati gari lake likiwa linasukumwa kutokana na kutafutwa.
“Wakati wanamfuata pale polisi walilazimika kutumia risasi baridi ndipo wafuasi wake wakafanikiwa kumtorosha kwa pikipiki,” alisema kamanda huyo.
CREDIT TANZANIA DAIMA.

BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES