Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

Archive

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

CHELSEA YAUTAFUTA MPIRA KWA TOCHI LAKINI YAAMBULIA SARE NYUMBANI KWA MANCHESTER UNITED.

No comments




MANCHESTER United na Chelsea zimetoshana nguvu kwa sare ya bila kufunguna kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

Mourinho akiiongoza Chelsea ndani ya Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu arejee kuikochi timu hiyo, alionekana kama mtu aliyelenga kujihami zaidi kuliko kusaka ushindi.

Kocha huyo ‘cha maneno’ akapanga kikosi kisicho mshambuliaji hata mmoja akiwa ni kocha wa kwanza kufanya hivyo katika histotia ya Ligi Kuu.

Mfungaji bora wa msimu uliopita Robin van Persie akashuhudiwa akipoteza nafasi muhimu zikiwa zimesalia dakika tatu kabla ya mchezo kukamilika baada ya shuti lake kuwababatiza Gary Cahill na John Obi Mikel.

Jose Mourinho hakufanya siri juu ya kuonyesha utashi wake wa kutaka kumsaini Wayne Rooney katika siku saba zijazo.
 
Akicheza nyuma ya washambuliaji, kinyume na Mourinho anavyotarajia kumtumia katika Chelsea, mshambuliaji huyo wa Uingereza, aling’ara vilivyo katika mechi hiyo ya kwanza kwake kuanza tangu mwezi April.
 
Rooney aliyekuwa akihaha uwanja mzima huku akishangiliwa na mashabiki wa pande zote mbili, alimjaribu kipa Petr Cech katika dakika za lala salama.
Chelsea tayari imeshuhudia ofa zake mbili za kutaka saini ya Rooney zikipigwa chini na sasa wanatarajiwa kupeleka ofa ya tatu baadae wiki hii.
 
Kama kuna mchezaji aliyeoneka anangeweza kufungua mlango wa magoli basi ni Rooney lakini hilo halikuweza kutokea na timu hizo zikalazimika kugawana pointi ambayo kwa namna yoyote ile hakuna upande ambao utasononeshwa na matokeo hayo.


Kwa mshangao wa wengi Mourinho akampiga benchi Juan Mata ambaye mashabiki wa United wangeridhika kumuona akibadilishwa na Rooney. Torres naye akaanzia benchi.

Kwa kiasi kikubwa United walitawala mchezo, wakipiga pasi nyingi na kulisogelea lango la Chelsea kila mara lakini mipango yao ikawa inatibuliwa na safu ya ulinzi ya Chelsea iliyokuwa ikiongozwa na John Terrey huku mipira michache ikiishia kwenye mikono Petr Cech.
 
Moja ya mashuti mazuri yaliyopigwa kwenye mchezo huo ni lile la Eden Hazard aliloliachia ubali wa mita 30 lakini likaokolewa na De Gea.
 
Pande zote mbili zililalamikia kunyimwa penalti, Cleverley alipiga mpira ulimogonga mkononi Frank Lampard, huku Ashley Cole akipelekwa chini na Phil Jones ndani ya box.
Kuingia kwa Torres kulishindwa kuleta mabadiliko yoyote yale.
 
Man United: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia (Young 67), Cleverley, Carrick, Welbeck (Giggs 78), Rooney, Van Persie.

Akiba: Anderson, Smalling, Lindegaard, Kagawa, Buttner,
Young.

Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne (Torres 60), Oscar, Hazard (Azpilicueta 93), Schurrle.

Akiba: Essien, Mikel, Lukaku, Schwarzer, Mata.
HABARI NA SAID MDOE - Saluti 5
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES