Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

Archive

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

MAKOSA 10 AMBAYO HUFANYWA NA WANAWAKE WANAPOKUWA FARAGHA NA WAPENZI WAO

No comments

Kitanda kina kanuni zake. Kuna makosa mengi hufanywa na wanawake, vilevile yapo ambayo wanaume huyafanya. Si sawa kuyaacha yaendelee kuwepo kwa sababu faragha ni hatua muhimu katika ukamilishaji wa kitu kinachoitwa penzi.

Uhusiano wa kimapenzi una wigo mpana. Kuna mambo mengi ambayo yakifanywa huufanya mwili uwe na afya. Hata hivyo, suala la faragha halipaswi kusahaulika, kwa maana ni chachandu madhubuti.

Tendo la faragha lina nguvu sana katika kuuweka hai uhusiano. Wapo watu ambao picha zilikuwa haziendi katika maisha ya kawaida lakini kila wakikutana kitandani, kila mmoja alimvulia kofia mwenzake.

Hii ina maana kuwa inawezekana mwenzi wako akawa dhaifu katika maeneo mengine lakini ‘maujuzi’ yake faragha, yakakufanya uwe mtulivu kwake.

Vivyo hivyo, nawe hakikisha unampatia mwezi wako katika eneo fulani ili hata akikufanyia visa, basi uwe na ukurasa wako ambao akiufikia ni lazima akuvulie kofia. Faragha ni uwanja huru ambao ambao hudhaniwa ni mgumu lakini ni rahisi sana.

Haihitaji msuli mkubwa wala nguvu kama za samba. Usidanganyike kwenda kutumia madawa ya kuongeza nguvu wala kwenda kwa waganga eti ndiyo wakuboreshee mvuto wako. Tuliza kichwa, soma kitendo chenyewe halafu hakikisha hufanyi makosa.

Katika makosa mengi ambayo wanawake huyafanya wakiwa faragha, ndani ya mada hii, nimeyaunganisha na kuyafanya yasomeke 10. Nikuhakikishie kuwa ukiyaepuka na kufuata mwongozo sahihi, utakuwa bora sana.

Mambo mengi hayahitaji taaluma, ni suala la kuushirikisha ubongo ili uamue kinachotakiwa. Mathalan; kuzungumza na mwenzi wako kumuuliza nini umfanyie ili afurahie tendo au kumwelewesha cha kufanya aweze kukupatia, haihitaji maarifa mengi au uwezo wa juu kiakili.
Kujifanya unajua sana husababisha wengi kuchemka. Achana na tabia ya kuhisi wewe umekamilika na kujidanganya kwamba unafahamu kila kinachotakiwa katika uwanja mahsusi wa faragha. Inakugharimu kiasi gani kuzungumza naye ili akujuze mahali hisia zake zilipolalia?
Yupo mwanamke ambaye tangu anazaliwa mpaka anakua, amekariri kwamba ukiwa faragha dawa ni kuzungusha ‘bakuli’ mwanzo mwisho. Matokeo yake, anakutana na mwenzi wake, badala ya kusoma mahitaji yake, yeye akili, nguvu na ujuzi wake wote anauelekeza katika nyonga tu. Mauno mtindo mmoja.
Hajui kwamba pengine mwenzi wake hapendi purukushani za kupanda na kushuka. Inapotokea wewe ni mtaalamu wa kucheza juu ya msumari (wana wa unyago mnaelewa), dakika 90 hushushi mzigo chini, ukidhani unamfurahisha, kumbe unageuka kero kwa mwezio.
Inaweza kutokea umekariri kuwa ukiwa katika utekelezaji wa sanaa ya faragha lazima uporomoshe mayowe. Japo ni nzuri katika kupata mrejesho (feedback) wa tendo lenyewe lakini si ajabu mwenzako hafurahii hilo. Zungumza naye tafadhali.
Hekima za tendo zinakataa ububu, lazima muwe mnaambiana mara kwa mara. Kama siku hajakutendea haki, mweleze waziwazi kwamba hajakufikisha. Ukimwacha afanye anachotaka na anachojisikia yeye, mwishowe haitakuwa na msisimko kwako.
Tengeneza utofauti wa makutano ya mbuzi na binadamu. Maana beberu huwa hajui maana ya kumwandaa jike. Anapojisikia kupanda anafanya hivyo na anapotosheka anashuka. Wewe na mwenzi wako hamna budi kuwa na nidhamu. Hisia ziheshimiwe.
Ikiwa mtatenda kwa makubaliano, kila mmoja akifuata maelekezo ya mwenzi wake, akitilia mkazo yale maeneo ambayo yametajwa katika mazungumzo kwamba ndiyo huleta raha, basi raha huwa raha kweli. Zingatia mambo 10 yafuatayo;

Itaendelea wiki ijayo.

GPL
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

WEMA SEPETU BILA KAJALA NAJIONA MTUPU

No comments


KASUMBA ya wanawake wengi kuwaambia mashoga zao siri zao nzito inadaiwa kumfanya msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu kufunguka kuwa, bila kuwa karibu na Kajala Masanja itakuwa ni kama kuamua kutembea mtupu.

                                             Wema Sepetu na Kajala Masanja.
Wema alifikia hatua ya kutoa maneno hayo katikati ya wiki hii kwa kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonesha yeye, meneja wake Martin Kadinda na Kajala huku akisindikiza na ujumbe mzito uliosomeka:
 
“I always call my poch and I fell so naked without, I need her everywhere with me. I hope that’s how they out each other.”
Aliandika kimombo, alimaanisha nini?
Tafsiri ya maneno hayo ni kwamba, Wema anamchukulia Kajala kama pochi yake na bila yeye anajihisi yuko uchi kiasi kwamba anataka kila sehemu wawe wote.

No comments :

Post a Comment

MATUKUO:LULU MICHAEL KATIKA UZINDUZI WA MUVI YAKE YA FOOLISH AGE NDANI YA MLIMANI CITY.

No comments
1




Elizabeth Michael (Lulu) akiwasili kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam tayari kwa uzinduzi wa filamu yake inayokwenda kwa jina la Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion chini ya Mwenyekiti wake Jonson
Lukaza ambaye ameweza kujitolea kwa hali na mali mpaka kufanikisha utengenezaji wa filamu hii na uzinduzi kwa ujumla, Uzinduzi huo unafanyika usiku wa kuamkia leo.

No comments :

Post a Comment

UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPA

No comments



Kundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajili ya onyesho hilo. Wasanii hao  8 ni kati ya 12 watakaopanda katika jukwaa moja uwanja wa Lake Tanganyika siku ya Jumamosi. Kundi la pili la wasanii ambao ni Profesa Jay, Diamond, Lady Jaydee na Barnaba wanatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi asubuhi.
Baada ya kupata mlo wa mchana ulioandaliwa na mwenyeji wao ambaye ni  Doctor Gerrard Mipango wasanii hao walipata nafasi ya kutembelea makumbusho ya Doctor Livingistone yaliyoko Ujiji na kujionea historia mbalimbali ya mzungu huyo anayetambuliwa kama mvumbuzi wa Ziwa Tanganyika na pia kuona maeneo biashara ya utumwa ilipokuwa ikifanyika na kujifunza kuhusu asili ya wenyeji wa Mkoa wa Kigoma.
 Mwasiti, Ben Pol na Roma baada ya kutua uwanja wa ndege wa Kigoma
 Fid Q, Kala Jeremiah na DJ Choka eneo la abiria waliowasili uwanja wa ndege
 Fid Q akitoka nje ya uwanja wa ndege
 Roma Mkatoliki akiondoka eneo la uwanja wa ndege
 Recho akijielekeza kwenye usafiri kuelekea hotelini
 Izzo Bizness akitoka uwanja wa ndege wa Kigoma
 Mtoto wa Kigoma Linex alikuwa wa mwisho kutoka nje ya uwanja wa ndege wa Kigoma
Baada ya kufanya ziara wasanii walipata nafasi ya kufanya manunuzi katika soko la Kigoma
 Wasanii wakipata mlo wa mchana nyumbani kwa Askofu Gerrard Mipango mjini Kigoma
 Wakali wa muziki katika picha ya pamoja na wenyeji wao mkoani Kigoma
Wasanii wakiwa katika eneo la mbele ya makumbusho ya Doctor Livingstone
Roma Mkatoliki akisaini kitabu cha wageni kwa niaba ya wasanii wengine

Wasanii wakimsikiliza mtaalam wa historia ya makumbusho ya Doctor Livingstone
 Mwasiti akisoma njia zilizotumika wakati wa biashara ya utumwa.

 Mtaalam wa historia akiwaonyesha wasanii mavazi ya wenyeji wa zamani wa mji wa Ujiji

Fid Q kama anajaribu kuwapatanisha Dr Livingstone na mwenzake.

 Wakazi wa Kigoma wakiwaangalia wasanii wakati wakifanya manunuzi soko kuu la Kigoma
 Muuzaji viatu akiwakaribisha wakali wa muziki kuangalia mzigo
Mashabiki hawa hawakutaka kupoteza nafasi ya kuonyesha upendo kwa Fid Q
 Wasanii wakirejea kwenye basi lao ambalo lilikuwa limezongwa na mashabiki
Mwasiti katika picha ya pamoja na mashabiki waliomuomba
"Konda" wa basi la wasanii Mwasiti akifunga mlango kwa ajili ya kurejea hotelini walikofikiaBONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

"SINA MPANGO WA KUACHANA NA DIAMOND NA SIJAONA MWANAUME KAMA YEYE"....PENNY

No comments


Baada ya hivi karibuni kuandikwa habari iliyoeleza kwamba nchini Kenya kuna demu aliyemzimikia ile mbaya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku akiahidi kumpa penzi zito, mpenzi wa msanii huyo Pe

No comments :

Post a Comment

VIDEO YA YALIO JIRI UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA DIAMOND "NUMBER ONE"

No comments


     DIAMOND AKI ONGEA NA WAANDISHI WA HABARI



Penny Mungilwa - Number 1 Video Launch





BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA FILAMU FIVE EFFECT "MTITU" ROHO MKONONI! SOMA KISA HAPA

No comments


SIKU chache baada ya kutangaza kuanza kusambaza filamu, Mkurugenzi wa Five Effect ametishiwa usalama na watu wasiojulikana.

Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, Mtitu alipoingiza filamu yake ya Omega mapema Jumatatu hii, watu wanaodaiwa kuwa ni wamiliki wa kampuni ya kusambaza kazi za wasanii wamemtishia kuwa wana mpango wa kumdhuru yeye ili asiendelee na kazi hiyo.
“Wamepitisha meseji ya vitisho kupitia kwa watu wao wa karibu ambao ni marafiki zangu, wakanitonya kuwa wana mpango wa kuniangamiza ili nisiwaharibie biashara yao,” alisema Mtitu na kuongeza:
“Kimsingi mimi simuogopi mtu, baada ya hii Omega natarajia kuingiza filamu ya Nyati ambayo itatoka siku si nyingi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

RAY C AFUTA YA MASANJA, NAE AOKOKA KWA KUBATIZWA CHECK TUKIO ZIMA

No comments


Yule dada yetu msanii maarufu wa nyimbo za ubongo wa fuleva leo hii amewaka bayana ya kuwa yeye na shetani sasa ni paka na panya. Amethibitisha hayo katika post zake za instagram. Wambea hatuna maneno mengi zaidi ya kusema angalia picha hizo na wote tuseme AMEN umechagua njia njema.
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti ya leo August 30 2013

No comments
.

No comments :

Post a Comment

MAJAMBAZI YA PORA SH 900 MILIONI BENKI HAPO JANA ASUBUHI

No comments


Suleiman Kova 

  • Alisema mmoja wa majambazi hao alikuwa ni mtu mwenye asili ya Asia na kwamba walikuwa wakizungumza Kiingereza kuwasiliana.

Dar es Salaam. Watu wanane wanaodhaniwa kuwa majambazi, jana walipora zaidi ya Sh900 milioni katika Tawi la Benki ya Habib, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Wizi huo ulitokea saa tatu asubuhi kwenye benki hiyo iliyoko makutano ya Mitaa ya Livingstone na Uhuru.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alisema fedha zilizoibwa ni Sh700 milioni na Dola za Marekani 181,885 (Sh285,444,000).
Kamanda Kova alisema wameanza kuwasaka majambazi hao waliohusika katika tukio hilo.
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Kova alisema majambazi hao walifika kwenye benki hiyo na kuingia ndani moja kwa moja na kujifanya ni wateja ambao walikuwa wamesindikizwa na mtu mmoja aliyekuwa amevaa sare za polisi.
Baada ya kuingia ndani, alisema waliwaweka chini ya ulinzi wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na wateja wanne waliokuwepo ndani wakipata huduma.
“Wananchi waliokuwa nje ya benki hawakujua chochote kinachoendelea huku dereva wa teksi aliyeambatana nao akipewa jukumu la kuangalia ulinzi nje huku akiwa na ‘radio call’,” alisema Kova.
Alisema mmoja wa majambazi hao alikuwa ni mtu mwenye asili ya Asia na kwamba walikuwa wakizungumza Kiingereza kuwasiliana.
Kamanda Kova alisema majambazi hao walikuwa yanafahamu majina ya watumishi wa benki hiyo akiwamo Meneja wake, Daniel Matemba jambo ambalo lilirahisisha kutekeleza uhalifu wao.
“Cha ajabu walianza kuwaita majina watumishi wawili pamoja na meneja na kuwaamuru watoe funguo za chumba cha kuhifadhia fedha baada ya kuchukua fedha zilizokuwa karibu,” alisema Kamanda Kova na kuongeza kuwa licha ya meneja huyo kuambiwa na wafanyakazi wake atoe taarifa kwenye Kampuni ya Ulinzi ya Security Group inayohusika na kulinda benki hiyo kwa kubonyeza kitufe maalumu alishindwa na badala yake kutii amri ya majamabazi hao.
Kamanda Kova alisema licha ya baadhi ya milango ya vyumba kufunguliwa kwa siri, ilikuwa ni kazi nyepesi kwa majambazi kuingia na kuchukua walichohitaji pasipo wananchi waliokuwa nje kujua kinachoendelea.
“Baada ya kuchukua fedha hizo majambazi hao walitoka nje kama vile wanatoka bafuni kuoga, yaani bila wasiwasi wowote na waliingia kwenye gari lao na kutokomea kiulaini,” alisema Kamanda Kova.
Alisema polisi imetangaza dau la Sh100 milioni kwa mtu atakayefanikisha kupatikana kwa taarifa za kukamatwa kwa majambazi hao.
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Mwanajeshi JWTZ auawa Kongo

No comments

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI JENERALI DAVIS MWAMU NYANGE


 Mashirika. Mpiganaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ Khatibu Mshindo aliuawa kwa kupigwa bomu juzi na waasi wa M23 kwenye Mji wa Goma ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano makali.
Wakati Mshindo ambaye alikuwa miongoni mwa askari wa Tanzania wanaounda Jeshi la Umoja wa Mataifa akifikwa na mauti, wapiganaji wengine 10 walijeruhiwa.
Askari wa Tanzania na wale wa Afrika Kusini wako DRC kwa kazi ya kulinda amani. Malawi bado haijapeleka majeshi yake.
Meja Mshindo alikuwemo katika kikosi cha vifaru na alikuwa kwenye Kambi ya 83KJ iliyoko Kiluvya Dar es Salaam.

No comments :

Post a Comment

PICHA:TAZAMA PICHA 50 ZA UZINDUZI WA NYIMBO MPYA YA DIAMOND NA JINSI ALIVYOTOA ZAWADI YA GARI KWA MSANII MSTAAFU "MZEE GURUMO"

No comments

Diamond Platnumz jana alifanya uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya, Number 1 kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo ndugu zake, marafiki, wasanii wenzake na wadau mbalimbali wa muziki nchini.
Chege Chigunda akifuatilia kwa makini
Chege Chigunda akifuatilia kwa makini
Kwenye uzinduzi huo pia, Diamond alimpa zawadi ya gari msanii mkongwe aliyetangaza kustaafu muziki, Muhidin Gurumo kama heshima kwake.
Diamond akienda kumkabizi Mzee Muidin Ngurumo Gari
Diamond akienda kumkabidhi Mzee Muhidin Gurumo gari
Diamond akimuonyesha Mzee Ngurumo Gari ambayo amemzawadia
Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari aliyomzawadia

Diamond akiongea na wadau walio fika
Diamond akiongea na wadau waliofika
Dully Sykes akiwa na Diamond wakiongea machache
Dully Sykes akiwa na Diamond wakiongea machache

Hao ndugu na Marafiki katika picha ya Pamoja
Ndugu na Marafiki katika picha ya pamoja
Hapa Diamond akimkabidhi Mzee Ngurumo Funguo ya Gari
Hapa Diamond akimkabidhi Mzee Gurumo funguo ya gari

Hapa Diamond akiongea machache na wasanii wenzake waliyo fika kumpa sapoti
Diamond akiongea machache na wasanii wenzake waliofika kumpa sapoti
Hili ndo Gari alilo pewa zawadi Mzee Ngurumo na Diamond
Hili ndo gari alilopewa Mzee Gurumo na Diamond
Hivyo ndivyo watu walivyo jitokeza kuja kuona New Video ya My No 1
Hivyo ndivyo watu walivyojitokeza kuja kuona video ya Number 1

Kama kawa burudani ilikuwepo kidigo
Kama kawa burudani ilikuwepo kidogo
Mzee Ngurumo akijaribu kidogo kupiga lesi baada ya kukabidhiwa Gari
Mzee Gurumo akijaribu kidogo kupiga lesi baada ya kukabidhiwa gari

Mzee Ngurumo akiongea machache na kumshukuru Diamond kwa kumpatia hiyo zawadi ya gari
Mzee Gurumo akiongea machache na kumshukuru Diamond kwa kumpatia zawadi ya gari
Nay wa Mitego akiwa pamoja na Madam Ritta
Nay wa Mitego akiwa pamoja na Madam Rita

Qeen Darleen na Bi Sandra
Queen Darleen na Bi Sandra
Rey Kigosi akifuatilia kwa makini sana
Ray Kigosi akifuatilia kwa makini sana

Wadau mbali mbali walio pata mualiko wakifuatilia
Wadau mbalimbali waliopata mualiko wakifuatilia
Wadau wa burudani wakifuatilia
Wadau wa burudani wakifuatilia

Wadau wakisubiri kwa hamu kuona kuona Video ya My no 1
Wadau wakisubiri kwa hamu kuona kuona video ya Number 1
watu wakifuatilia
Watu wakifuatilia

Asha Baraka,Qeen Darleen pamoja na Mama Diamond Bi Sandra
Asha Baraka,Queen Darleen pamoja na Mama Diamond
IMG_5498
IMG_5500
IMG_5510
IMG_5516
IMG_5517
IMG_5520
IMG_5522
IMG_5524
IMG_5525
IMG_5526
IMG_5527
IMG_5533
IMG_5534
IMG_5535
IMG_5537
IMG_5540
IMG_5541
IMG_5548
IMG_5554
IMG_5557
IMG_5558
IMG_5561
IMG_5564
IMG_5575
IMG_5579
IMG_5582
IMG_5586
IMG_5588
  IMG_5506
IMG_5507
IMG_5531
IMG_5505
IMG_5523
IMG_5546
IMG_5512
IMG_5567
IMG_5568
IMG_5518
IMG_5519
IMG_5572

BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES