Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

Archive

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

Kisa Ngassa, Yanga yaishtaki TFF Uswis.

No comments


KWA ufupi ni kama Yanga imesema: “Kama noma na iwe”, hiyo ni baada ya kutoa kauli kuwa imekata rufaa ya kufungiwa kwa mchezaji wao, Mrisho Ngassa, kucheza mechi sita na kulipa Shilingi milioni 45 ambapo imeamua kulipeleka suala hilo kwa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas) iliyopo Uswis.
 
Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, amesema licha ya kuwa rufaa yao ipo mikononi mwa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), lakini kuna kila dalili kuwa Simba wamemsajili mchezaji huyo ‘kimagumashi’, hivyo adhabu za Fifa zipo wazi kuwa viongozi wa timu hiyo wanatakiwa kufungiwa siyo chini ya miezi 12.
 
Alisema wanaamini Ngassa ni mchezaji wao halali na watapeleka malalamiko yao Cas ikiwa wataona haki haijatendeka, kwani wanaamini Ngassa amefungiwa kwa vifungu ‘hewa’.
 
Mwalusako amesema adhabu iliyotolewa haijataja vifungu vya sheria ya kumwadhibu 
Ngassa, pia kama ni kweli alisaini mkataba na Simba, kwa vile mikataba iliyopo inaonyesha alifanya hivyo kabla ya kipindi cha miezi sita ya mkataba wake wa Azam kumalizika, hivyo Simba nao walikiuka sheria na wanastahili kuadhibiwa.
 
“Sheria za usajili zinasema mchezaji anaweza kusaini makubaliano na timu nyingine akibakiza miezi sita kabla ya mkataba wake wa awali kufikia tamati, lakini karatasi zilizopo zinaonyesha Ngassa alisaini mkataba huo wa Simba kabla ya kipindi hicho kufika.
 
“Maana yake kama ni adhabu hata Simba wanatakiwa kuadhibiwa, lakini kumfungia mchezaji kucheza mechi sita ni kuiadhibu Yanga kwa kosa ambalo halihusiki.
 
“Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ambayo imetoa adhabu hiyo haijaweka wazi kifungu cha kanuni Yanga au Ngassa waliyokiuka. Yanga inaiona adhabu hii kuwa ni ya uonevu kwa klabu na mchezaji, hivyo tumeshawasilisha barua ya pingamizi tangu Agosti 23, 2013,” alisema Mwalusako.
 
Mwalusako ameeleza kuwa mazingira yaliyokuwepo na kuripotiwa kwenye vyombo vya habari likiwemo suala la usajili wa mchezaji huyo kutoka Azam kwenda Simba na kipindi alipotaka kusajiliwa na El Merreikh, yanaonyesha Ngassa alikuwa akilazimishwa kufanya maamuzi mengi.
 
“Ngassa alikataa kwenda Simba kwa kudai kuwa hawezi kuuzwa kama mbuzi, yaani bila kushirikishwa, baadaye alitishwa kuwa kama asingeenda Simba basi angekaa benchi mpaka mwisho wa mkataba wake.
 
“Suala la kujiuliza ni kwa nini mkataba waliosaini Simba na Azam tarehe 2/8/2012, haukuizuia Simba kupinga uuzwaji huo? Jibu ni rahisi kwamba mkataba haukuwa na nguvu yoyote ya kikanuni au kisheria, ndiyo maana Simba hawakupinga.
 
“Mwongozo wa Fifa juu ya hadhi za wachezaji na masuala ya kinidhamu kipengele cha 3(d) unaeleza kuwa katika kuhakikisha udhibiti wa mkataba baina ya mchezaji na klabu, mahusiano ya kiajira lazima yazingatie uwiano wa pande zote mbili.
 
“Kifungu cha 3(f) cha mwongozo huo kinabainisha kuwa kuna vipindi viwili tu vya usajili katika msimu mmoja. Je, Simba waliingia makubaliano na Ngassa katika kipindi kipi mbali na kuwa katika mkopo kwa msimu mmoja?
 
“Ngassa hakuwa na mkataba halali na Simba, inakuwaje awajibishwe kinidhamu na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwa makubaliano ambayo hayatambuliwi kikanuni na kisheria?
 
“Lakini pia Ngassa hakupewa nafasi ya kujitetea juu ya utata wa yanayosemekana makubaliano ya  kumpa fedha. Kama ilithibitika Ngassa kapokea fedha, ni kiasi gani? Na kama alipewa gari, thamani yake ni kiasi gani? Hivyo vyote huthibitishwa kwa risiti au ‘bank statement’,” alisema.
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES