Dk. Slaa kunguruma Gongo la Mboto kesho.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.
Willibrod Slaa, pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho
wanatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara Gongo la Mboto, Dar es
Salaam kesho Jumamosi.
Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam jana,
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Ukonga, Jumaa Mwipopo, alisema mkutano huo
utakaofanyika katika viwanja vya Kampala utaanza saa tisa alasiri, na
kuwataka wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao kuhudhuria kwa
wingi, wakiwamo viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali.
Mwipopo alisema lengo la ujio wa kiongozi huyo wa kitaifa wa chama hicho ni kuhutubia mkutano huo kuhusu mabaraza ya Katiba.
Viongozi wengine wanaotarajiwa kufuatana na Dk. Slaa ni Mbunge wa
Jimbo la Ubungo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John
Mnyika, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mjumbe wa Kamati Kuu na
Mwanasheria wa chama hicho, Mabere Marando na wengine wengi.
Vilevile Mwipopo alisema katika mkutano huo uongozi wa CHADEMA Jimbo
la Ukonga utagawa rasimu za Katiba bure kwa wananchi wote
watakaohudhuria na vijitabu vinavyohusu mapendekezo ya Katiba mpya ya
CHADEMA.
Akizungumzia kuhusu mkutano mkuu wa jimbo uliofanyika Agosti 18, 2013
ambao ulihusu mapendekezo ya CHADEMA kuhusu Katiba waitakayo Watanzania,
alisema ulikuwa wenye mafanikio, kwa sababu watu mbalimbali bila kujali
itikadi za vyama vyao maoni yao yalisikilizwa na kuzingatiwa.
Mwipopo alisema katika mkutano huo aliwahimiza Watanzania kuchangia
maoni yao kwa kina kuhusu Katiba mpya, akibainisha kuwa umaskini
tulionao umetokana na ubovu wa Katiba.
Alishutumu sera mbovu zilizopo za ‘kuwabeba’ wageni (wawekezaji), kwa
serikali kuwamilikisha ardhi na kuwaacha wananchi wanyonge wakiteseka
bila kuwa na sauti kuhusu ardhi yao inayochukuliwa.
“Mwekezaji anapokuja kutoka nje na anataka kuwekeza katika ardhi, aje
moja kwa moja kwa mwananchi mwenye ardhi hiyo na aingie naye mkataba
mwananchi mwenyewe. Huu ndio moja ya mipango ya CHADEMA ili kumpa
mwananchi uwezo wa kumiliki rasilimali ya nchi yake. Lakini tutafanya
hivyo kwa kufuta kipengele cha kusema ardhi ni mali ya serikali,”
alisisitiza Mwipopo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**
Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPAKundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
-
Klabu ya Arsenal io mbioni kukamisha usajili wa kiungo wa Real Madrid Mesut Ozil katika siku ya mwisho ya usajili barani ulaya. ...
No comments :
Post a Comment