HII NDIO HISTORIA YA TRAFIC FEKI ALIEKAMATWA KINYELEZI JIJINI DARA,! SOMA HAPA UJUE ALIKOANZIA UTAPELI WAKE
SIKU
chache baada ya kukamatwa kwa askari 'feki' wa Usalama Barabarani
mwenye cheo cha Sajini, akifanya kazi ya kuongoza magari eneo ya Tabata
Kinyerezi, Dar es Salaam, mambo mapya yamezidi kubainika juu ya sababu
za mtu huyo kujiingiza katika kazi hiyo bila kutambuliwa na Jeshi la
Polisi.
Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vya kuaminika, zinasema trafiki huyo 'feki', ambaye inadaiwa jina lake halisi ni James Juma Hussein (45), mkazi wa Kimara Matangini, alianzia kazi hiyo mkoani Singida kabla ya kujipa uhamisho wa kikazi kwenda Dar es Salaam.
Chanzo
chetu kilieleza kuwa, trafiki huyo alikuwa na shemeji yake aliyeitwa
Shaban ambaye aliajiriwa na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama
Barabarani aliyekuwa akifanyia kazi mkoani Tabora.Vyanzo
vyetu viliongeza kuwa, baada ya shemeji yake kufariki mkoani Tabora,
trafiki huyo alipata mwanya wa kuchukua nguo za kazini alizokuwa
akizitumia shemeji yake.
Inadaiwa
trafiki huyo 'feki', aliwahi kupata mafunzo ya upolisi katika Chuo cha
Polisi Moshi (CCP), mkoani Kilimanjaro lakini alifukuzwa.Chanzo
hicho kiliongeza kuwa, baada ya ndugu wa trafiki huyo kufariki dunia,
trafiki 'feki', alikuwa akifanya kazi hiyo bila ndugu zake kujua
akianzia mkoani Singida bila kushtukiwa.
"Jamaa
aliamua kujirithisha kazi ya shemeji yake, alikwenda Singida na kufanya
kazi hiyo kwa muda usiojulikana," kilisema chanzo chetu.Chanzo
hicho kiliongeza kuwa, kutokana na uchache wa matrafiki mkoani Singida,
aliingiwa hofu ya kuweza kujulikana; hivyo aliamua kujipa uhamisho wa
kwenda jijini Dar es Salaam.
"Akiwa
Dar es Salaam, alifanya kazi hii kwa muda mrefu bila kujulikana hadi
alipokamatwa wiki iliyopita akiwa eneo lake la kazi akiongoza magari,"
kilisema chanzo hicho.Mtoa habari huyo alisema polisi walianza kumtilia shaka trafiki huyo kutokana na adhabu zake alizokuwa akizitoa kwa madereva.
"Tulianza
kuwa na hofu naye kwa sababu yeye adhabu zake kwa kila dereva aliyekuwa
akimkamata alimtoza sh. 20,000 hadi 25,000," kilieleza chanzo hicho.Sababu
nyingine iliyowafanya polisi wamtilie shaka ni utamaduni wake wa
kuondoka mapema kwenye kituo cha kazi ambavyo alikuwa akijipangia
mwenyewe.
"Trafiki
akiwa kazini, inabidi awe kituoni kwake kuanzia asubuhi hadi jioni muda
wa kazi unapomalizika, tulishangaa kuona mwenzetu anaingia kazini
asubuhi na kuondoka kabla ya muda wa kazi," kiliongeza chanzo hicho.Inadaiwa
trafiki huyo alikuwa akifanya hivyo baada ya kukamilisha mahesabu yake
aliyokuwa amejiwekea ambapo hali hiyo iliwafanya polisi waanze kujiuliza
maswali na ndipo walipoanza kumfuatilia.
Baada
ya kufuatiliwa bila yeye kujua, walibaini hata upigaji wake wa saluti
ni utata mtupu ambapo kutokana na hali hiyo, waliweka mtego na
kufanikiwa kumkamata.
Hadi sasa anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi ambalo limeahidi kutoa taarifa kamili baada ya uchunguzi wao kukamilikaBONGO NEWS 4 NEWS#
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**
Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPAKundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
-
Klabu ya Arsenal io mbioni kukamisha usajili wa kiungo wa Real Madrid Mesut Ozil katika siku ya mwisho ya usajili barani ulaya. ...
No comments :
Post a Comment