WILAYA ya Arumeru mkoani Arusha kujenga uwanja wa kisasa wa soka.
WILAYA ya Arumeru mkoani Arusha iko mbioni kujenga uwanja mkubwa
wa kisasa wa soka ikiwa ni mpango mkakati wa kuendeleza michezo
wilayani hapa baada ya kufanikiwa kuwa na timu nyingi za vijana.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo (DC), Nyerembe Munasa,
wakati akizungumza katika hafla ya utoaji zawadi kwa mabingwa wa ligi
maalumu ya vijana Arumeru, iliyoanzishwa na mdau wa michezo kutoka
nchini Ufaransa, Damian Sellier, katika mji mdogo wa Usa River, eneo la
Liganga.
DC Nyerembe alisema, hiyo ni mikakati yake katika kukuza michezo kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Meru, ambako tayari eneo la ujenzi
limepatikana na kinachofuata ni mipango ya ukusanyaji fedha kwa ajili ya
ujenzi huo kuanza.
Alifafanua kuwa katika mpango huo, kabla ya ujenzi kukamilika, hivi
sasa wataanzisha mashindano ya vijana wadogo kutafuta vijana 20 bora,
ambao watakuwa waanzilishi wa timu maalumu ya wilaya, ambayo mwakani
itapelekwa nchini Brazil kwa ajili ya mafunzo maalumu.
“Tayari nimeishapata baadhi ya wadhamini kusaidia mpango wa kukuza
soka kwa vijana na tumekubaliana kuanzia na vijana 20, ambao watapelekwa
nchini Brazil kwa ajili ya mafunzo maalumu, ili wakirudi wawe ndio
mfano kwa soka la nchi hii,” alisema Munasa.
Aidha, kupitia Halmashauri ya Meru, waliahidi mara baada ya kumalizika
kwa mashindano hayo juzi, wataanza kuukarabati uwanja wa Ngarasero, kwa
kuukwangua na kuweka udongo mpya kisha kupanda majani ili uwe na hadhi
stahiki kutumika katika mechi mbalimbali.
Naye Mratibu wa kituo cha Usa River Youth, ambao ndio walikuwa
wasimamizi wa ligi hiyo, Daudi Mkumba, licha ya kumshukuru DC Nyerembe
na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru kwa ushirikiano wao, aliwaomba
kuhakikisha wanatoa ushirikiano zaidi kwa taasisi zinazoanzisha
mashindano ya vijana ili kukuza na kuibua vipaji.
Katika mashindano hayo, timu ya Charky U-20 na ile ya U-15 waliibuka
mabingwa na kuambulia kombe na mipira, kabla ya DC Nyerembe kutoa sh
200,000.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**
Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
-
A still from the video in which Yemeni girl Nada Al-Ahdal pleaded with parents not to arrange marriages for their young children, b...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
UMEONA PICHA ZA WASANII WATAOTUMBUIZA KIGOMA KATIKA KILL TOUR WALIPOWASILI KIGOMA? BASI ZICHEKI HAPAKundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajil...
No comments :
Post a Comment