ALEX MASSAWE AFUNGULIA KESI YA KUGHUSHI
*Mahakama
yaamuru arejeshwe Tanzania
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,imetoa hati ya kukamatwa na kurejeshwa nchini
mfanyabiashara maarufu nchini Alex
Siliyamala Massawe ili aje kukabiliana na kesi yake mpya ya kughushi nyaraka za
umiliki wa ardhi na kutoa taarifa za uongo.
Amri hiyo
imetolewa na Hakimu Mkazi Gene Dudu muda mfupi baada ya wakili Mwandamizi wa
serikali Tumaini Kweka kuwasilisha ombi hilo mahakamani na kuiarifu mahakama
kuwa upande wa jamhuri umemfungulia kesi Massawe na.150/2013 ya kughushi hati za
umiliki wa ardhi na kutoa nyaraka za uongo mahakamani hapo na kumsomea
mashashitaka Massawe ambaye anashikiliwa na Askari wa Interpol Dubai bila ya
Massawe kuwepo mahakamani hapo .
Hakimu Dudu
alisema anakubaliana na ombi hilo la wakili Kweka na kwamba mahakama yake
imetoa amri ya kukamatwa kwa Masawe kokote alipo na arejeshwe nchini ili aje
akabiliane na kesi yake hiyo mpya iliyofunguliwa mahakamani hapo.
Aidha Hakimu
Dudu alisema pia anakubaliana na ombi la wakili Kweka lilokuwa linaiomba
mahakama hiyo itamke majina sahihi yanayotumiwa na Massawe hata kama
kule Dubai anakoshikiliwa na
askari wa Interpol anatumia majina mengi, ambapo hakimu Dudu alisema
majina halali ya Massawe ni Alex Siliyamala Massawe ambayo ndiyo yaliyoandikwa
kwenye hati ya mashitaka ya kesi hiyo Na.150 ya mwaka huu.
Hivi
karibuni vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Interpol cha Jeshi la Polisi
hapa nchini , Babile alithibitishia vyombo vya habari kuwa Massawe amekamatwa
na askari wa Interol huko Dubai kwa tuhuma mbalimbali.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Agosti 24 mwaka 2013
BONGO NEWS 4 NEWS#- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Total Pageviews
328700
About Us
Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.
Recent Posts
Ads 468x60px
Blog Archive
Followers
IN ENTERTAINMENT
SERENGETI FIESTA 2013 MKOANI MTWARA NOOOOOMAAAA SAAAANAAAAA
Wakazi wa Mtwara wajitokeza kwa wingi katika Tamasha la Burudani la...SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA, DIAMOND APOKONYWA PASSPORT.., MASANJA MKANDAMIZAJI NAYE YUPO
Ni mwendelezo wa Sakata la unga ambalo sasa ni janga kwa taifa letu. Orodha...VIDEO YA YALIO JIRI UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA DIAMOND "NUMBER ONE"
DIAMOND AKI ONGEA NA WAANDISHI WA HABARI Penny Mungilwa - Number 1...
ADVERTISE MENT
**ADVERTISE MENT**

Pages
VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )
STAR VOTE
TOP HEAD LINES
-
Muda au Pesa Nyingi!" Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kuanzisha mahusiano ya karibu...
-
PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake ...
-
MUZIKI ni kazi, mataifa mengi, hususan katika mabara ya Ulaya na Amerika Kaskazini, ume...
-
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwa...
-
Kujichua au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako hur...
No comments :
Post a Comment