Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

Archive

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

SERIKALI YAKAMATA MADINI YENYE THAMANI YA HELA NDEFU LIVE UWANJA WA NDEGE, CHEKI HAPA

No comments



SERIKALI kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini, imekamata madini ya vito yenye thamani ya Sh bilioni 13.17, yaliyokuwa mbioni kutoroshwa nje ya nchi. Madini hayo yalikamatwa katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini, ikiwa ni pamoja na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro na Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TMAA, Bruno Mteta, alisema madini hayo yalikamatwa kwa kipindi cha kuanzia Septemba 2012 hadi Julai, 2013.

Mteta alisema matukio ya utoroshwaji wa madini yamekuwa yakihusisha wageni zaidi, huku akitaja madini yanayoongoza kutoroshwa kwenda nje ni Tanzanite (vito), Amber, Green Gunnet, Soil and gold, Red gold moon stone na Green Tomalin.

Mteta alisema biashara ya kusafirisha madini nje ya nchi kwa njia za magendo, hivi sasa imeshamiri nchini na kuifananisha na biashara haramu ya usafirishaji wa dawa za kulevya.

“Biashara hii hufanywa sana na raia wa nje, hatukatai watu wasifanye biashara ya madini, lakini wafuate utaratibu unaokubalika.

Zipo kesi zinaendelea mahakamani na kesi nyingine zipo mikononi mwa polisi kwa uchunguzi, lakini zipo kesi tatu tayari hukumu imetolewa na madini kutaifishwa,” alisema Mteta.

Mteta alisema Agosti 20, mwaka huu, raia mmoja wa kigeni (hakumtaja jina wala uraia), alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akiwa na aina mbali mbali za madini yenye thamani ya Sh. milioni 25.32.

Mteta alisema siku hiyo hiyo, TMAA kwa kushirikiana na polisi walimkamata raia mwingine wa kigeni katika makazi yake, Jangwani Beach, akiwa na madini ya vito vya thamani.

Uthaminishaji wa madini hayo unaendelea, japokuwa yanaonekana kuwa na thamani kubwa sana, mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi,” alisema.

Alisema TMAA ipo katika hatua za mwisho kuweka mtambo wa kisasa katika viwanja vyote vya ndege, utakaosaidia kubaini watu wanaotorosha madini kwenda nje ya nchi.

“Ni vigumu sana kubaini mtu akiwa amebeba madini, sababu hakuna sauti inayotoka pale mtuhumiwa anapopita kwenye mashine za usalama kwenye viwanja vya ndege, ikilinganishwa na dawa za kulevya au kitu cha hatari,” alisema.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES