Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

Archive

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

Azam : Kiboko ya vigogo

No comments

 
 
KWA misimu miwili mfululizo ni kama Azam FC imekuwa haina bahati. Imekuwa ikiishia kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na kushiriki Kombe la Shirikisho.
Timu hiyo tajiri yenye kila kitu kinachostahili kuitwa timu ya kisasa ya kulipwa, imejipanga kivingine tayari kwa msimu mpya. Msisitizo wa kocha ukiwa ni kuchukua kombe na kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa vile Shirikisho sasa imetosha.
Kocha huyo Mwingereza, Sterwart Hall hakufanya mabadiliko kwenye kikosi chake lengo likiwa ni kuendeleza makali waliyoanza msimu uliokwisha. “Nataka kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita na kuvunja rekodi ya mwaka uliopita, ndiyo malengo yetu,” anasema Stewart ambaye timu yake ndiyo klabu pekee ya Tanzania iliyokwenda Afrika Kusini kwa mechi za kirafiki na ilidumu huko kwa siku kumi.
Katika mechi za huko, safu ya ushambuliaji ndiyo iliyomwangusha kwa kushindwa kufunga mabao mengi jambo ambalo linaonekana kuwa ni tatizo kwenye kikosi hicho. “Mabao ni tatizo, lakini tutacheza na hesabu tu pamoja na mazoezi na kufanikisha malengo yetu na kila mchezaji atafunga,” anafafanua.
Azam, ambayo Jumamosi iliyopita ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii, itaanza ligi bila wachezaji wake wa kimataifa, raia wa Kenya, Humphrey Mieno anayeumwa nyama za paja na Brian Umony raia wa Uganda anayeuguza maumivu ya enka.
Kikosi cha Azam
Azam ipo chini ya Mkurugenzi Aboubakary Bakhresa na makazi yao ni Chamazi, Mbande, jijini Dar es Salaam, ina miaka sita tangu ilipoanzishwa lakini imekuwa tishio kwa wakongwe Simba na Yanga.
Kwa misimu miwili mfululizo mwaka juzi na mwaka jana, iliwapangua wakongwe hao, ikawaweka pembeni na kung’ang’ania nafasi ya pili kwenye ligi na kuliwakilisha Taifa mara mbili Kombe la Shirikisho.
Pia, licha ya ugeni wao huo ndiyo klabu pekee Tanzania inayomiliki uwanja wao binafsi wa kisasa wenye ‘pichi mbili’, moja nyasi bandia na mwingine una nyasi asilia pamoja na hosteli. Mtibwa ndiyo klabu nyingine  yenye uwanja binafsi wenye nyasi asilia. Hali hiyo inaifaidisha Azam ambayo itacheza mechi nyingi zaidi kwenye uwanja wao wa nyumbani ambao pembeni kidogo zipo hosteli zao zinazotumika kwa kambi.
Stewart anasaidiwa na Kalimangonga Ongala pamoja na Mkenya, Ibrahim Shikanda kwenye benchi la ufundi. Kocha Stewart ambaye kwa hulka yake ni mcheshi, amebainisha kuwa mfumo anaopenda kuutumia ni 4-3-3 ingawa mara nyingine ni 4-2-3-1 na 4-1-2-3.
Nahodha wa timu ni John Bocco ‘Adebayor’ na Himid Mao ndiyemsaidizi wake.  Straika, Gaudence Mwaikimba, ndiye mchezaji mrefu kuliko wote na Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ ni mchezaji mfupi kuliko wote katika kikosi hicho.
Azam itatumia jezi za nyumbani rangi nyeupe na ugenini ni bluu na njano.

Azam haijafanya usajili wowote, lakini imewapandisha wachezaji wanne kutoka timu B ya vijana chini ya miaka 20 ambao ni kipa Aishi Manula, Mudhahir Yahya, Hamad Kadili na Dismas.
Wachezaji wa kimataifa ni pacha kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche na Kipre Bolou, Wakenya Mieno na Jockins Atudo pamoja na Brian Umony raia wa Uganda.
Wazawa ni Mwaikimba, Himid, Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aziz, Bocco, Khamis Mcha, Luckson Kakolaki, Mwadini Ally, Said Morad, Marika Ndeule, David Mwantika, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Sure Boy, Samih Haji, Waziri Salum na Seif Karihe.

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES