Recent Posts

coments

HOT HEAD LINES

NEWS+HABARI-ZAIDI

Archive

ALL HERE DONE BY |

ALL HERE DONE BY |

**ADVERTISEMENT**

**ADVERTISE**

**ADVERTISE**

HAPPY BIRTH DAY

HAPPY BIRTH DAY
Powered by Blogger.

Dk. Slaa kunguruma Gongo la Mboto kesho.

No comments


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho wanatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara Gongo la Mboto, Dar es Salaam kesho Jumamosi.

Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam jana, Katibu wa CHADEMA Jimbo la Ukonga, Jumaa Mwipopo, alisema mkutano huo utakaofanyika katika viwanja vya Kampala utaanza saa tisa alasiri, na kuwataka wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao kuhudhuria kwa wingi, wakiwamo viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali.
Mwipopo alisema lengo la ujio wa kiongozi huyo wa kitaifa wa chama hicho ni kuhutubia mkutano huo kuhusu mabaraza ya Katiba.
Viongozi wengine wanaotarajiwa kufuatana na Dk. Slaa ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwanasheria wa chama hicho, Mabere Marando na wengine wengi.
Vilevile Mwipopo alisema katika mkutano huo uongozi wa CHADEMA Jimbo la Ukonga utagawa rasimu za Katiba bure kwa wananchi wote watakaohudhuria na vijitabu vinavyohusu mapendekezo ya Katiba mpya ya CHADEMA.
Akizungumzia kuhusu mkutano mkuu wa jimbo uliofanyika Agosti 18, 2013 ambao ulihusu mapendekezo ya CHADEMA kuhusu Katiba waitakayo Watanzania, alisema ulikuwa wenye mafanikio, kwa sababu watu mbalimbali bila kujali itikadi za vyama vyao maoni yao yalisikilizwa na kuzingatiwa.
Mwipopo alisema katika mkutano huo aliwahimiza Watanzania kuchangia maoni yao kwa kina kuhusu Katiba mpya, akibainisha kuwa umaskini tulionao umetokana na ubovu wa Katiba.
Alishutumu sera mbovu zilizopo za ‘kuwabeba’ wageni (wawekezaji), kwa serikali kuwamilikisha ardhi na kuwaacha wananchi wanyonge wakiteseka bila kuwa na sauti kuhusu ardhi yao inayochukuliwa.
“Mwekezaji anapokuja kutoka nje na anataka kuwekeza katika ardhi, aje moja kwa moja kwa mwananchi mwenye ardhi hiyo na aingie naye mkataba mwananchi mwenyewe. Huu ndio moja ya mipango ya CHADEMA ili kumpa mwananchi uwezo wa kumiliki rasilimali ya nchi yake. Lakini tutafanya hivyo kwa kufuta kipengele cha kusema ardhi ni mali ya serikali,” alisisitiza Mwipopo.
BONGO NEWS 4 NEWS#

No comments :

Post a Comment

Total Pageviews

About Us

Spice Mag - Premium free blogger template developed by spicytricks.com.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Maecenas hendrerit iaculis nunc. Curabitur in eros ipsum. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas. Duis at mi justo, non suscipit elit. Nunc aliquam luctus adipiscing. Nullam sit amet lacus vitae odio congue mollis eu non magna. Duis sed arcu a libero adipiscing rhoncus. Aliquam erat volutpat. Suspendisse sed nunc metus, sed aliquet arcu.

Ads 468x60px

Blog Archive

Followers

IN ENTERTAINMENT

ADVERTISE MENT

**ADVERTISE MENT**

**ADVERTISE MENT**

VIDEO OFTHE DAY (Diamond Platnumz - Number One (Official Video Music) )

TOP HEAD LINES